Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Dkt Juliana Pallangyo wakati wa uzinduzi wa mradi wa umeme wa Solar kwenye Kijiji hicho ambao utasaidia wananchi kuondokana na
changamoto ya upatikanaji wa huduma hiyo muhimu
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Dkt Juliana Pallangyo wa kwanza kushoto akipiga makofi mara baada ya uzinduzi wa mradi wa umeme wa Solar kwenye Kijiji hicho ambao utasaidia wananchi kuondokana na changamoto ya upatikanaji wa huduma hiyo muhimu
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini,Dkt Juliana Pallangyo katika akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali kushoto Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert Gabriel mara baada ya uzinduzi wa mradi wa umeme
wa Solar kwenye Kijiji hicho ambao utasaidia wananchi kuondokana na changamoto ya upatikanaji wa huduma hiyo muhimu
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati
na Madini,Dkt Juliana Pallangyo akicheza ngoma wakati wa wa uzinduzi wa mradi wa umeme wa Solar kwenye Kijiji hicho ambao utasaidia wananchi kuondokana na changamoto ya upatikanaji wa huduma hiyo muhimu
WANANCHI wa Kijiji cha Mpale Kata ya Mpale wilayani Korogwe Mkoani Tanga wametakiwa kutumia nishati ya umeme waliopatiwa kwa shughuli za uzalishaji mali ikiwemo kuanzisha viwanda vidogo vidogo na miradi itakayoweza kuwaingizia fedha ili kujikwamua kiuchumi wao na jamii zao.
Hayo yalisema mwishoni mwa wiki na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini,Dkt Juliana Pallangyo wakati wa uzinduzi wa mradi wa umeme wa Solar kwenye Kijiji hicho ambao utasaidia wananchi kuondokana na changamoto ya upatikanaji wa huduma hiyo muhimu.
Mradi huo umefadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji na Maendeleo (The United Nations Capital Development Fund-UNCDF), ikishirikiana na kampuni ya Ensol Tanzania Ltd. (Ensol) hivyo kuwezesha umeme katika eneo hilo kwa mara ya kwanza.
Alisema uwepo wa nishati hiyo kwenye kijiji hicho utafungua fursa nyengine kwa wananchi kuweza kujikwamua kimaendeleo kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo vya kusagia nafaka, mashine za useremala na kutengeneza samani.
“Licha ya hivyo lakini pia wataweza kufanya uchomeaji wa vyuma ambapo kwa kufanya hivyo ninyi wananchi wa hapa mpale mtakuwa mnaenda sambamba na mwamko mpya wa Tanzania ya Viwanda”Alisema Dkt Pallangyo.
Alisema upatikanaji wa nishati hiyo kwa wananchi hao ni maendeleo makubwa yaliyopatikana katika kipindi kifupi tangu wakala wa nishati vijiji ulipoanzioshwa mwaka 2005.
“Serikali sasa kupitia wakala wa Nishati imezindua rasmi mpango wa tatu wa kusambaza umeme maeneo ya vijijini na tumeweka lengo la kufikia vijiji vyote ifikapo mwaka 2022.
Awali akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradiu huo, Msimamizi Mkuu wa Mradi huo, Prosper Magali alisema alisema shughuli za mradi huo zilianza rasmi Machi mwaka 2014 baada ya kutembelea kijiji hicho pamoja na vyengine vilivyopo wilayani Korogwe.
Alisema licha ya kutembelea wilaya hiyo lakini pia walitembelea maeneo mengine Tanzania kutafuta vijiji na maeneo yanayofaa kwa miradi ya uzalishaji mdogo wa umeme kwa kutumia teknologia ya umeme wa Jua.
Aidha alieleza waliamua kuanza mradi wa mfano katika kijiji hicho
baada ya kuwa kijiji bora kwa vigezo walivyoweka vya kiuchumi, kijamii na kimakjazi ukilinganisha na vyengine walivyotembelea.
“Shughuli ya mradi zilifuatiwa na zoezi la kufanya upembuzi yakinifu, Mpango wa kibiashara (Bussines Plan) pamoja na makadirio ya kiufundi mambo ambayo yalitusaidia kuandaa nyaraka za kuwasilisha kwa wafadhili na wawekezaji mbalimbali “Alisema.
“Baada ya hapo mmwaka 2014 mwishoni, Taasisi ya Energy and Environment Partnership (EEP) Program yenye makao yake makuu huko Pretoria nchini Afrika kusini inayopata ufadhili wa Serikali za Finland,Uingereza na Austria kupitia mpango wake wa kutoa ufadhili wa miradi ya nishati endelevu kwa nchi za kusini na mashariki ya Africa kwa mtindo wa ushindani.
“June 10 mwaka 2015 tuliweza kusaini makubaliano rasmi ya EEP ya ufadhili wa miaka miwili wa mradi huu uliokuwa na thamani ya Euro 263,000 ikiwa ni asilimia 63 ya gharama za mradi “Alisema.
Aliongeza kuwa bado wanaendelea na zoezi la kutafuta fedha zaidi za kutekeleza mradi huo lakini kwa bahati nzuri baada ya mazungumzo ya muda mfupi, Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo ya Mitaji (United Nations Capital Development Fund ya UNCDF).
Aliongeza kuwa baada ya mazungumzo hayo taasisi hiyo ilikubali kutoa asilimia 22 ya gharama za mradi USD 124,000 na walitiliana saini ya makubaliano ya ufadhili wa fedha hizo Novemba mwaka 2015.

EmoticonEmoticon