KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA MABORESHO YA BANDARI YA TANGA

March 13, 2026





Na Oscar Assenga,TANGA

Kamati ya kudumu ya Bunge ya miundombinu leo imefanya ziara ya kutembelea Bandari ya Tanga huku ikiridhinshwa na uboreshaji wa miundombinu katika Bandari ya Tanga hatua inayoonesha mabadiliko ya kiutendaji ikiwemo ongezeko la shehena za mizigo.

Hayo yalisemwa leo na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Joyce Ndalichako wakati wa ziara hiyo katika Bandari ya Tanga ambapo alisema maono ya Serikali yameleta mapinduzi katika Bandari ya Tanga na wao kama wasimamizi wataendelea kuisimamia Serikali katika utekelezaji wa mradi huo



Uboresho huo wa Bandari ya Tanga umepelekea kuvuka lengo la upokeaji wa shehena za mizigo kutoka mataifa mbalimbali kutoka tani 137,000 mwezi Oktoba hadi kufikia tani zaidi ya 200,000 mwezi Novemba mwaka 2025.



Alisema kutokana na maboresho hayo wana kila sababu ya kuipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Raisi Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uboreshaji wa Bandari ya Tanga hatua inayochagiza kuinua uchumi wa mkoa wa Tanga kwa kiasi kikubwa.




Profesa Ndalichako alisema kwamba uwekezaji huo wa shilingi bilioni 429.1 uliofanywa na Serikali katika Bandari ya Tanga umewezesha uchimbwaji wa kina na ujenzi wa gati hatua iliyoiongezea ufanisi wa utendaji na hivyo kuwezesha meli kubwa kutia nanga na kurahisisha shughuli za upakiaji na upakuaji wa mizigo.

Aliongeza Serikali ina maono ya kuunganisha Bandari na reli ambapo mpango uliopo ni kujenga reli ya kisasa ya SGR kutoka Tanga hadi Musoma hatua itakayochochea maendeleo ya mkoa wa Tanga na kuzalisha ajira kwa vijana.



Kamati ya kudumu ya Bunge ya miundombinu imeipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Raisi Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uboreshaji wa Bandari ya Tanga hatua inayochagiza kuinua uchumi wa mkoa wa Tanga kwa kiasi kikubwa.

Uwekezaji wa shilingi bilioni 429.1 uliofanywa na Serikali katika Bandari ya Tanga zimewezesha uchimbwaji wa kina na ujenzi wa gati na hatimaye kuleta ufanisi wa utendaji katika Bandari hiyo hatua inayowezesha Meli kubwa kutia nanga na kurahisusha shughuli za upakiaji na upakuaji wa mizigo.



Aidha katika hatua nyengine Profesa Ndalichako amesema Serikali ina maono ya kuunganisha Bandari na reli ambapo mpango uliopo ni kujenga reli ya kisasa ya SGR kutoka Tanga hadi Musoma hatua itakayochagiza maendeleo ya mkoa wa Tanga hususani kwa vijana kupata ajira.



Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, alisema Serikali inaendelea na mpango wa kuunganisha bandari hiyo na mtandao wa reli wa kilomita 248 (Tanga–Mruazi–Ruvu) na hatimaye kufika Arusha.



Alisema pamoja na kuwa na reli ya SGR kupitia Minjingu na Engaruka hadi Musoma itakuwa kiunganishi muhimu cha kiuchumi.

Naye kwa upande wake ,Meneja wa Bandari ya Tanga, Salehe Mbega alisema maboresho hayo yameongeza kina cha maji kufikia mita 12 hali inayoruhusu meli kubwa zenye urefu wa hadi mita 200 kutia nanga gatini tofauti na hapo awali.


Share this

Related Posts

Previous
Next Post »