NAIBU WAZIRI ARDHI AITAKA NHC KUONA NAMNA YA KUANZISHA MIRADI MIKUBWA KILA WILAYA NCHINI

March 15, 2026



Na Oscar Assenga,TANGA


NAIBU Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi,Kaspar Mmuya amelitaka Shirika la Taifa la Nyumba (NHC) waanze kufikiria namna ya kuanzisha miradi mikubwa ambayo inaweza kutoa huduma kwa wananchi kwenye kila mikoa na wilaya ili wajipambanue utofauti wao na mashirika mengine.

Mmuya aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea mradi wa Jengo la Kitega Uchumi unaosimamiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Mkwakwani Plaza ambapo alisema kutokana na uwepo wa mahitaji yake kwa wananchi waliopo maeneo mbalimbali hapa nchini.

Mradi huo ni moja ya miradi mingi NHC wanafanya nchini na unagharimu kiasi cha Sh.Bilioni 8.6 fedha ambazo zilizopitishwa na Bunge katika Bajeti ya Mwaka 2025/2026 ambapo ulianza mwaka jana mwezi wa sita na utakamilika kwa muda wa miezi 24 na wanategemeaJune mwakani utakamilika .

Mpaka sasa mradi huo umetekelezwa kwa asilimia 37 na fedha zilizotumika ni zaidi ya Bilioni 2 ambao utakuwa na ghorofa tatu za mwanzo za biashara za kawaida,ya pili na tatu ni kutakuwa na ofisi mbalimbali na ya nne mpaka nane hizo ni kwa ajili ya makazi watajenga nyumba 20 ambazo nyumba 10 zitakuwa na vyumba viwili pamoja na master, jiko na vitu vingine na vyumba 10 zitakuwa na vyumba vitatu.

“Kwa kweli nimetembelea mradi huu nimeridhika kwa maana nimeona thamani ya fedha iliyotumika mpaka asilimia ya utekelezaji kuna uwiano mkubwa nimeangalia ubora na umahiri wa mafundi waliokuwepo nimejiridhisha kuna unadhifu mkubwa kwenye kazi yao”Alisema Naibu Waziri huyo.

Alisema pia ujenzi wa Jengo hilo umezingatia mazingira rafiki kwa watu wote kwamba litakuwa na lifti mbili ambazo zitatoa huduma za kijamii katika ghorifa ya tatu na kuna lifti ambayo watakuwa wanatumia watu watakaokuwa wanakaa juu kwenye nyumba za makazi na nyumba hizo hazitakodishwa zitauzwa kwa mtu yoyote mwenye uwezo wa kununua na matangazo tiyari wamekwisha kuwekwa.

Alisema kuna umuhimu wa uwepo wa miradi kama hiyo katika wilaya mbalimbali ikiwezekana mradi unaofanana nao waweke kwenye majimbo yote 272 ili wakitembea wajumbe NHC wapo katika maeneo ambayo wapiga kura wa Rais,Wabunge na Madiwani wanapotokea lakini niwapongeze kwa mradi huu.

Hata hivyo alimshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu kwa kulifanya shirika hilo liwe imara kiuchumi lakini lijielewe sasa linabidi lisonge mbele katika kuwekeza zaidi katika ujenzi wa makazi.

Ambapo zaidi ya nyumba milioni 3 kila mwaka ni mapungufu ama mahitaji ambayo yanahitajika kwenye nchi na wanavyoelewa idadi ya watu inaongezeka kwa kiasi kikubwa na mahitaji ya nyumba yanaongezeka.

“Wito nyie wenyewe mmejionea mradi upo asilimia 37 na zaidi ya asilimia 70 ya Jengo hilo tayari watu wameanza kuchukua nafasi kununua hivyo kuna mahitaji makubwa ya nyumba hapa Tanga ushauri wangu anzeni kufikiri kuanza miradi mikubwa inayoweza kutoa huduma kwa wananchi ili kujipambanua na kujitofautisha na mashirika mengine “Alisema

Kwa upande wake Msimamizi mkuu wa Mradi huo kutoka NHC Ephahim Msigwa alisema mradi huo unatumia fedha za ndani na una ghorofa nane ambapo ghorofa tatu zitakuwa kwa ajili ya biashara na tano za makazi ya watu ambapo mpaka sasa wamekwisha kutumia Bilioni 2.1.

Mradi huo ni wa miaka miwili ambapo ulianza kutekelezwa mwezi juni mwaka 2025 na kwamba unatarajiwa kukamilika ukamilike mwezi juni 2027 ambapo mpaka sasa upo asilimia 37.9 huku wananchi zaidi ya 189 wa Mkoa wa Tanga wakinufaika na ajira kwenye mradi huo.

Mwisho

Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »