Showing posts with label CCM. Show all posts
Showing posts with label CCM. Show all posts

JUKWAA HURU LA WAHARIRI TANZANIA, UTPC KUSHIRIKIANA KUTETEA HAKI, MASLAHI YA WAANDISH

September 02, 2026 Add Comment

 

.



JUKWAA Huru la Wahariri Tanzania (JUWATA) na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) wamekubaliana kuimarisha ushirikiano katika kulinda uhuru wa vyombo vya habari, kutetea haki na maslahi ya waandishi wa habari pamoja na kuhakikisha jamii inapata habari sahihi na kwa wakati.


‎‎Makubaliano hayo yamefikiwa katika kikao cha pamoja cha viongozi wa JUWATA na UTPC kilichofanyika katika ofisi za UTPC zilizopo Barabara ya Aboud Jumbe, Mtaa wa Kazembo, eneo la Uzunguni jijini Dodoma.


‎Katika kikao hicho, viongozi hao walijadili masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya habari, ikiwemo umuhimu wa kuwa na mshikamano miongoni mwa wadau wa habari katika kukabiliana na changamoto zinazowakabili waandishi wa habari na vyombo vya habari nchini.


‎Aidha, walisisitiza umuhimu wa taasisi hizo kushirikiana katika kutetea uhuru wa vyombo vya habari, haki za waandishi wa habari na maslahi yao, huku wakitambua nafasi muhimu ya wanahabari katika kuhabarisha, kuelimisha na kuwajibika katika jamii.


‎Ushirikiano huo pia unalenga kuongeza nguvu katika kushughulikia changamoto zinazohusu mazingira ya kazi ya waandishi wa habari, pamoja na kujenga mahusiano mazuri kati ya wadau wa habari na taasisi mbalimbali zinazohusika na maendeleo ya sekta hiyo.


‎UTPC ina jumla ya Klabu 28 za Waandishi wa Habari zinazowakilisha waandishi wa habari kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, hivyo kuwa na mtandao mpana wa kuwafikia wanahabari katika maeneo mbalimbali nchini.


‎Kwa upande wa JUWATA, ujumbe uliongozwa na Mwenyekiti wake, Richard Mwaikenda, akifuatana na Makamu Mwenyekiti, Sylivester Ngombaniza, pamoja.


‎UTPC iliwakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji, Kenneth Simbaya, pamoja na Afisa wa Programu wa Ufuatiliaji Rasilimali, Andrew Malawiti, Kaimu Afisa wa Fedha Winfrida Madeni na Afisa Msaidizi wa Programu, Edmund Kapungu.


‎Viongozi hao wameeleza umuhimu wa kuendeleza mawasiliano na ushirikiano wa karibu baina ya taasisi hizo kwa manufaa ya waandishi wa habari, vyombo vya habari na jamii kwa ujumla.


‎Wamesisitiza kuwa mshikamano wa wadau wa habari ni muhimu katika kujenga sekta imara, yenye weledi na inayoweza kutekeleza kwa ufanisi wajibu wake wa kuhabarisha umma na kulinda maslahi mapana ya jamii.


‎ ...........,...............


‎Jukwaa Huru la Wahariri Tanzania (JUWATA) limeanzishwa kihalali kwa kuzingatia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, likiwa na lengo la kupanua wigo kwa Wahariri wanaotimiza vigezo kuwa huru kujiunga na jukwaa hilo, ili kuongeza nguvu, umoja na ushirikiano katika kutetea na kulinda haki na maslahi ya Waandishi wa Habari pamoja na jamii kwa ujumla.



‎Katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku, JUWATA itazingatia Katiba na kanuni zake, sambamba na kufuata na kuheshimu Sheria za Nchi pamoja na taratibu zinazotawala tasnia ya Habari.


‎Kwa ufupi, JUWATA haijaasisiwa kwa lengo la kupambana, kushindana au kusigana na taasisi nyingine za Habari.



‎Badala yake, inalenga kujenga ushirikiano, mshikamano na mahusiano mema na taasisi za Habari za ndani na nje ya nchi, kwa manufaa ya Wahariri, Waandishi wa Habari na jamii kwa ujumla.


‎JUWATA inaamini kuwa umoja, ushirikiano na kuheshimiana ndiyo msingi wa kujenga tasnia imara, huru, yenye uwajibikaji na inayoweza kusimamia kwa ufanisi haki na maslahi ya Wadau wa Habari.

Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC, Kenneth Simbaya (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa Jukwaa Huru la Wahariri Tanzania (JUWATA. Richard Mwaikenda pamoja na Makamu Mwenyekiti wa jukwa hilo, Sylivester Ngombaniza baada ya kufanya kikao hicho.



Kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa JUWATA,Ngombaniza,Kaimu Afisa wa Fedha, Winfrida Madeni, Mwenyekiti wa JUWATA, Mwaikenda, Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC, Simbaya na Afisa wa Programu UfutiliajiRasilimali, Andrew Malawiti.


Viongozi wa JUWATA na UTPC wakiwa katika kikao hicho.



Mwaikenda akimsikiliza kwa makini Simbaya wakati wa kikao hicho.

Mwaikenda akizungumza wakati wa kikao hicho.

Simbaya akiagana na viongozi wa JUWATA.

CCM YATHIBITISHA MSINGI WA KUHUDUMIA WANANCHI KWA VYAMA TAWALA AFRIKA

July 22, 2026 Add Comment

 

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Ndugu Rabia Abdalla Hamid , ameshiriki Mkutano Mkuu wa Chama cha Botswana National Front (BNF) unaofanyika mjini Jwaneng, Botswana, akiwakilisha Chama Cha Mapinduzi.


Akizungumza katika mkutano huo, Ndugu Rabia amesisitiza kuwa kila chama tawala kina wajibu wa kuwatumikia wananchi kwa uadilifu, kuimarisha misingi ya utawala bora, na kuendelea kutoa huduma zinazokidhi mahitaji ya wananchi bila kuchoka.


Aidha, amekisii Chama cha BNF kuendelea kuzingatia maslahi ya wananchi katika utekelezaji wa sera na maamuzi yake, pamoja na kuhakikisha kuwa hakuna mwananchi anayebaki nyuma katika mchakato wa maendeleo ya taifa.

Aidha,Ndg. Rabia amempongeza Rais wa Chama cha Botswana National Front (BNF) na Rais wa Jamhuri ya Botswana, Mheshimiwa Duma Gideon Boko kwa  ushindi wa Chama chake na kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Jamhuri ya Botswana. 


Ameeleza kuwa kuchaguliwa kwa Rais Boko na Chama cha BNF ni kielelezo cha imani waliyopewa na wananchi wa Botswana na  amewatakia mafanikio katika kuwaletea maendeleo  na ustawi wao.

CCM TANGA KUOKOA MILIONI 90 KWA UJENZI WA NYUMBA ZA WATUMISHI

April 14, 2026 Add Comment









Na Oscar Assenga, Tanga

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajab Abdurhaman amesema mkakati wao wa  ujenzi wa nyumba za watumishi kila wilaya ni hatua itakayosaidia kuokoa kiasi kikubwa cha fedha zilizokuwa zikitumika kulipia pango.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua miradi ya chama mkoani humo, mwenyekiti huyo alisema ameridhishwa na hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa nyumba hizo, akiwapongeza wadau wote walioshiriki kuchangia mradi huo.

“Kwa ujumla mmefanya kazi kubwa sana. Nawashukuru wadau wote walioshiriki, kwa sababu walichotoa si msaada tu, bali ni uwekezaji ambao utaendelea kuzaa matunda,” alisema.

Alifafanua kuwa kabla ya ujenzi huo, baadhi ya watumishi wa chama walikuwa wakilipa hadi shilingi 200,000 kwa mwezi kwa pango, huku wengine wakilipa zaidi, hali iliyokuwa ikiigharimu CCM kiasi kikubwa cha fedha kwa mwaka.

Alisema kwa makadirio ya haraka, chama kilikuwa kinatumia fedha nyingi kwa mwaka katika wilaya moja kwa ajili ya pango, na endapo wilaya zote za mkoa zitakamilisha ujenzi wa nyumba za watumishi, CCM itaokoa hadi shilingi milioni 90 kwa mwaka.

“Fedha hizi zitasaidia kufanya shughuli nyingine za maendeleo ndani ya chama. Huu ni ubunifu ambao umehimizwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa pamoja na Kamati Kuu,” aliongeza.

Aidha, alisema ujenzi wa nyumba hizo pia unalenga kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi wa chama, kwa kuhakikisha wanapata makazi bora na salama baada ya kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Alisisitiza umuhimu wa kuendelea na juhudi hizo ili kuhakikisha miradi yote inakamilika katika mkoa mzima wa Tanga, huku akieleza imani kuwa kwa ushirikiano uliopo, malengo hayo yatafikiwa.

Katika hatua nyingine, mwenyekiti huyo alielekeza kuhakikisha maeneo yote ya chama yanakuwa na hati miliki halali, pamoja na kulindwa kwa kupanda miti ya kivuli na matunda ili kuhifadhi mazingira na kuepusha migogoro ya ardhi.

Aliwataka viongozi wa chama ngazi ya wilaya kuhakikisha wanazingatia sheria za ardhi, ikiwa ni pamoja na kulipa kodi ya pango la ardhi na kufuata taratibu zote za umiliki.

Kwa upande wake, alisisitiza kuwa uwekezaji katika miundombinu ya chama ni muhimu kwa ustawi wa chama hicho,