Showing posts with label CCM. Show all posts
Showing posts with label CCM. Show all posts

CCM TANGA KUOKOA MILIONI 90 KWA UJENZI WA NYUMBA ZA WATUMISHI

April 14, 2026 Add Comment









Na Oscar Assenga, Tanga

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajab Abdurhaman amesema mkakati wao wa  ujenzi wa nyumba za watumishi kila wilaya ni hatua itakayosaidia kuokoa kiasi kikubwa cha fedha zilizokuwa zikitumika kulipia pango.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua miradi ya chama mkoani humo, mwenyekiti huyo alisema ameridhishwa na hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa nyumba hizo, akiwapongeza wadau wote walioshiriki kuchangia mradi huo.

“Kwa ujumla mmefanya kazi kubwa sana. Nawashukuru wadau wote walioshiriki, kwa sababu walichotoa si msaada tu, bali ni uwekezaji ambao utaendelea kuzaa matunda,” alisema.

Alifafanua kuwa kabla ya ujenzi huo, baadhi ya watumishi wa chama walikuwa wakilipa hadi shilingi 200,000 kwa mwezi kwa pango, huku wengine wakilipa zaidi, hali iliyokuwa ikiigharimu CCM kiasi kikubwa cha fedha kwa mwaka.

Alisema kwa makadirio ya haraka, chama kilikuwa kinatumia fedha nyingi kwa mwaka katika wilaya moja kwa ajili ya pango, na endapo wilaya zote za mkoa zitakamilisha ujenzi wa nyumba za watumishi, CCM itaokoa hadi shilingi milioni 90 kwa mwaka.

“Fedha hizi zitasaidia kufanya shughuli nyingine za maendeleo ndani ya chama. Huu ni ubunifu ambao umehimizwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa pamoja na Kamati Kuu,” aliongeza.

Aidha, alisema ujenzi wa nyumba hizo pia unalenga kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi wa chama, kwa kuhakikisha wanapata makazi bora na salama baada ya kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Alisisitiza umuhimu wa kuendelea na juhudi hizo ili kuhakikisha miradi yote inakamilika katika mkoa mzima wa Tanga, huku akieleza imani kuwa kwa ushirikiano uliopo, malengo hayo yatafikiwa.

Katika hatua nyingine, mwenyekiti huyo alielekeza kuhakikisha maeneo yote ya chama yanakuwa na hati miliki halali, pamoja na kulindwa kwa kupanda miti ya kivuli na matunda ili kuhifadhi mazingira na kuepusha migogoro ya ardhi.

Aliwataka viongozi wa chama ngazi ya wilaya kuhakikisha wanazingatia sheria za ardhi, ikiwa ni pamoja na kulipa kodi ya pango la ardhi na kufuata taratibu zote za umiliki.

Kwa upande wake, alisisitiza kuwa uwekezaji katika miundombinu ya chama ni muhimu kwa ustawi wa chama hicho,