HABARI

SIASA

ELIMU

Recent Posts

ASKOFU DKT.SHOO AKEMEA UPOTOSHAJI MCHANGO WA RAIS SAMIA KWA TAASISI ZA DINI

July 04, 2025 Add Comment

Mwenyekiti wa CCT, Askofu Dkt. Fredrick Shoo amesema kuwa baadhi ya watu kwa sababu zao binafsi wamekuwa wakidai kuwa msaada wa Rais, Dkt. Samia ni sehemu ya hongo, madai ambayo yamekuwa yakimuumiza sana kama kiongozi wa dini. Niendelee kumsihi Rais Samia asirudishwe nyuma na watu hao bali aendelee kuwa na hofu ya Mungu katika kusaidia huduma za kiroho nchini. 

Askofu Mkuu Shoo amebainisha hayo Julai 03, 2025 Jijini Dodoma wakati wa Mkutano Mkuu wa 32 wa Jumuiya ya Kikristo nchini Tanzania - CCT ambapo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko alimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano huo.

BENKI YA CRDB YASHINDA TUZO YA DHAHABU YA KIMATAIFA YA UWEKEZAJI KATIKA JAMII KUPITIA CRDB MARATHON

July 04, 2025 Add Comment

 

Benki ya CRDB imeshinda tuzo ya dhahabu ya Kimataifa ya Uwekezaji katika Jamii (International CSR Awards 2025) kupitia mbio zake za kimataifa ya CRDB BANK International Marathon.

Tuzo hii ya hadhi ya juu imetolewa na CSR Society, shirika huru la kimataifa linalotambua na kuenzi mashirika yenye juhudi za uwajibikaji wa kijamii duniani kote lenye makao makuu yake nchini Uingereza.
Mwaka huu, Benki ya CRDB ilikuwa miongoni mwa washiriki 300 walioshindana kutoka nchi mbalimbali duniani na kushinda tuzo hiyo kwa kuonyesha ubunifu mkubwa katika uwezeshaji wa kijamii katika nyanja tofauti.

Akiiwakilisha Benki ya CRDB na kupokea tuzo na cheti cha ushindi, Afisa Uwekezaji wa Jamii, Natalia Tuwano amesema tuzo hii inaipa Benki ya CRDB heshima na hadhi ya juu katika kuiwezesha jamii na makala yake kuhusu jambo hilo kubwa yatachapishwa na Jarida la Viongozi wa Uwezeshaji Jamii Duniani – rejeleo la kimataifa la mazoea bora ya uwajibikaji wa kijamii. Hii pia inaruhusu benki kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Green World Awards mwakani ujao.
“CRDB Bank International Marathon ni mfano wa jinsi juhudi za kijamii zinavyoweza kuleta mabadiliko chanya na kuimarisha jamii zetu,” amesema Natalia. “Tunawashukuru CSR Society kwa kutambua jitihada zetu na tunaahidi kuendelea kutekeleza mipango inayolenga maendeleo endelevu ya kijamii.”

Benki ya CRDB imekuwa mstari wa mbele katika kukuza afya, elimu, uendelevu wa mazingira, na mshikamano wa kijamii kupitia kampeni hii ambayo imevutia maelfu ya watu kutoka makundi mbalimbali.

UDOM Yaja na Mashine ya Kuuza Vinywaji Inayojiendesha

July 03, 2025 Add Comment
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), kupitia Ndaki ya Sayansi za Kompyuta na Elimu Angavu, kimebuni mashine ya kisasa ya kuuza vinywaji baridi inayojiendesha yenyewe bila kuhitaji uwepo wa mtu kwa ajili ya kutoa huduma kwa mteja.

NEEC WAJA NA FURSA ZA KIUCHUMI KATIKA MAONEHO YA 49 YA KIMATAIFA YA BIASHARA (SABA SABA)

July 03, 2025 Add Comment
Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) linashiriki katika maonesho ya 49 ya kimataifa ya Biashara katika banda la Ofisi ya Waziri Mkuu na watakuwepo hapo kipindi chote cha maonesho ili kuwawezesha Watanzania.

MRADI WA BOMBA LA GESI NTORYA–MADIMBA KUGHARIMU SHILINGI BILIONI 120

July 03, 2025 Add Comment
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limesaini mkataba wa makubaliano na kampuni ya China ya CPP na CPTDC kwaajili ya ujenzi wa bomba la gesi asilia kutoka Ntorya hadi Madimba mkoani Mtwara kwa kipindi cha miezi 12.

TBS YAWASILISHA UTEKELEZAJI WA SERA YA KURUDISHA KWA JAMII

July 03, 2025 Add Comment
EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limepokea tuzo kutoka Taasisi ya Foundation for Disabilities Hope, kutokana na desturi waliyojiwekea kutoa mchango wao kwa watu mbalimbali hususani jamii ya watu wenye ulemavu.

SADC YAITAJA TANZANIA KINARA UTEKEKEZAJI AJENDA YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

July 03, 2025 Add Comment


📌 *Rais Samia aendelea kupongezwa kwa kuwa kinara wa Nishati safi ya Kupikia Afrika*


📌 *Mhe. Kapinga ataka mikakati, ubunifu utekelezaji nishati safi ya Kupikia Jumuiya ya  SADC*


📌 *Asisitiza uelimishaji matumizi ya nishati safi ya kupikia kupewa nguvu*


📌 *SADC yapongeza Tanzania mkutano wa Misheni 300*


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametajwa kuwa kinara namba moja wa uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi ya kupikia Afrika na Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya  Nishati na Maji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). 

Pongezi hizo zimetolewa leo Julai 3, 2025 na Viongozi mbalimbali na Wataalam kutoka Nchi nane za (SADC) ambao wamekutana jijini Harare nchini Zimbabwe katika Mkutano  unaolenga kuimarisha na kujadili masuala mbalimbali yatakayowezesha mtangamano wa Kikanda katika sekta za nishati na maji.

Akizungumza Katika mkutano huo, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema kuwa Serikali imeendelea kuwezesha, kuhamasisha na kutoa elimu kuhusu umuhimu wa matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kufikia malengo yaliyoainishwa kwenye mkakati wa kitaifa wa matumizi ya nishati safi ya kupikia (2024 – 2034).


Kuhusu utekelezaji wa nishati safi ya kupikia kwa jumuiya hiyo, Mhe. Kapinga ameitaka SADC kuweka dhamira na mikakati ya utekelezaji wa ajenda ya nishati safi ya kupikia ili kuwafikia watu wengi zaidi SADC. 

Vilevile, amesisitiza SADC kuwa wabunifu katika matumizi ya nyenzo mbalimbali zitakazowezesha na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia huku akitolea mfano matumizi ya mkaa mbadala kama vile wa rafiki briquettes katika matumizi ya kupikia kama njia ya kuhamasisha matumizi ya nishati hiyo kwa wananchi. 


Pia, Mhe. Kapinga ameitaka SADC kuweka nguvu zaidi katika uelimishaji na uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi ya kupikia na kuwataka wanachama wa SADC kuweka mkakati utakaowezesha unarahisisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kuwa muhimu kwa uchumi endelevu katika maeneo yao.



Katika hatua nyingine, Mhe. Kapinga amepokea pongezi zilizotolewa na Wanachama wa SADC kwa Tanzania kwa  kuandaa, kuwa mwenyeji na kufanikisha mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Nishati wa Afrika (Misheni 300 - M300) kwa ufanisi mkubwa uliofanyika jijini Dar es Salaam.


Naye, Waziri wa Nishati wa Malawi, Mhe. Ibrahim Matola amempongeza Rais Samia kwa uthubutu wake wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa Watanzania. Mhe. Matola ameitaka SADC kuitumia Tanzania kama balozi wa matumizi ya nishati safi ya kupikia katika jumuiya hiyo.


Mkutano huo umehudhuliwa na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Mhe. Suzan Kaganda, Wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati akiwemo Kamishna Msaidizi wa Maendeleo ya Umeme, Mha. Styden Rwebangila, Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mha. Hassan Saidy, Mkurugenzi wa  Mipango na Uwekezaji (TPDC), Derick Moshi, Mkurugenzi wa Mifumo ya Udhibiti Umeme (TANESCO) , Mha. Deogratius Mariwa, Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi (EWURA), Msafiri Mtepa na  Wataalam kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

NAIBU WAZIRI UMMY AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUGHARAMIA MAZISHI WALIOFARIKI SAME

July 03, 2025 Add Comment


Na Mwandishi Wetu - KILIMANJARO


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa moyo wake wa upendo  kwa kugharamia mazishi ya  miili  42 ya watu waliofariki dunia kufuatia  ajali iliyotokea  Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.

Mhe. Nderiananga ametoa shukrani hizo  tarehe 03 Julai, 2025 wakati aliposhiriki tukio la kuaga miili 35 katika viwanja vya Hospitali ya Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC) akisema miili Saba ilichukuliwa na ndugu zao na miili miwili bado vipimo vya DNA vinafanyiwa kazi ili kutambulika.

Tukio hilo lilioongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Nurdin Babu ambapo Mhe. Nderiananga alimpongeza kwa kujitoa kwa kiasi kikubwa tangu ilipotokea ajali hiyo akishirikiana na watendaji wake wote.

Amesema Serikali  kupitia Idara ya Menejimenti ya Maafa iliyopo Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Kilimanjaro kwa juhudi kubwa zilizofanyika kuokoa manusura wa ajali hiyo pamoja na miili ya walioungua kwa moto mara baada ya ajali kutokea.

Vilevile ameipongeza Serikali kupitia Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kuchukua  sampuli za miili hiyo (DNA)  kuhakikisha ndugu wanatambua miili ya wapendwa wao.

Hata hivyo  Mhe. Nderiananga ameendelea kutoa pole kwa Serikali, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia msiba huo mzito kwa Taifa  huku akiwaomba kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu hadi watakapokamilisha kuwahifadhi wapendwa wao. 



Aidha, ajali hiyo iliyotokea Juni 28 2025 katika Kitongoji Mahuu, Kata ya Same, takribani kilomita nne kutoka Same mjini, ililihusisha basi kubwa la abiria, Mali ya Kampuni ya Chanel One, lenye namba za usajili T 179 CWL na basi dogo la abiria aina ya Toyota Coaster, lenye namba T 199 EFX linalomilikiwa na Kampuni ya Mwami Trans.




Coaster hiyo, ilikuwa ikitokea Same kuelekea Manispaa ya Moshi, wakati basi la Chanel One lilikuwa likitokea Arusha kuelekea Tanga.

MIRADI YA NISHATI SAFI IACHE ALAMA KWA WANANCHI,ASEMA KAMISHNA LUOGA

July 03, 2025 Add Comment

 



*📌Afungua Mkutano wa Sita wa Kamati ya Uwekezaji miradi ya nishati safi ya kupikia*


*📌 Aishukuru EU na UNCDF kutekeleza ajenda ya nishati safi ya kupikia kwa vitendo*


*📌 Asema ushirikishwaji wa srkta binafsi ni chachu ya kuleta maendeleo miradi ya nishati safi*


*📌UNCDF kuangalia uwezekano wa kituo cha elimu kwa vitendo kuhusu nishati safi ya kupikia*


Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mha. Innocent Luoga amesema utekelezaji wa miradi ya nishati safi ya kupikia inapaswa kuweka alama kwa wananchi  ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa


Kamishna luoga ameyasema hayo leo julai 3 ,2025 wakati akifungua mkutano wa sita wa wa kamati ya uwekezaji miradi ya nishati safi ya kupikia unaotekelezwa kwa pamoja kati ya Serikali, Umoja wa Ulaya na Shirika la umoja wa mataifa la maendeleo na mitaji ili kusaidia utekelezaji wa miradi ya nishati safi ya kupikia

‘’Serikali kupitia Wizara ya Nishati na wadau wa nishati safi ya kupikia imefanya kazi kubwa kuhakikisha malengo yanatimia ikiwemo utekelezaji na ushirikishwaji wa sekta binafsi kwenye miradi ya nishati safi ya kupikia ili kubadili fikra na kutimiza azma ya Serikali ya kufikia asilimia 80 ya watanzania kutumia nishati safi ya kupikia ifikapo 2034’’ Amesema Mha. Luoga.

Amesema chini ya uwepo wa kamati hii ya uwekezaji kumekuwa na mafanikio mbalimbali ikiwemo uwekezaji kwenye teknolojia mbalimbali za miradi ya nishati safi ya kupikia ili kuwezesha wanachi kutumia teknolojia mbalimbali ikiwemo gesi,umeme, na mabaki ya kinyesi cha wanyama na kuachana na matumizi ya nishati isiyo safi

 


Kwa upande wake, Mratibu wa mradi kutoka UNCDF Bw. Emmanuel Muro amesema  UNCDF kupitia Cook fund chini ya ufadhili wa Umoja wa ulaya inaandaa mpango wa kuanzisha kituo maalum cha matokeo kwa vitendo ili kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa nishati mbalimbali zinazotumika kwa ajili ya matumizi ya kupikia ili wananchi wawe na uwelewa mpana juu ya nishati mbalimbali za kupikia

Mkutano huo wa sita wa wadau umepitisha wafanyabiashara wadogo 17 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya teknolojia ya nishati  safi ya kupikia kwa ajili ya ufadhili ili isaidie urahisishaji kwa watumiaji wa teknolojia ya nishati safi ya kupikia.



DC UPENDO WELLA AAPISHWA TABORA,AHAIDI USHIRIKIANO NA HUDUMA BORA KWA WANANCHI

July 03, 2025 Add Comment

 



Mkuu mpya wa Wilaya ya Tabora, Mhe. Upendo Wella, aapishwa rasmi na kuahidi kushirikiana na viongozi wa mkoa na wilaya  hiyo kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na maendeleo endelevu.

Katika hafla yenye heshima na uzito wa kiutawala iliyofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Upendo Wella ameapishwa rasmi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora. Uapisho huo umefuatia uteuzi uliofanywa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ikiwa ni sehemu ya mabadiliko ya kiutendaji ndani ya utumishi wa umma.

Mara baada ya kula kiapo chake cha utii, Mhe. Wella alitumia jukwaa hilo kumshukuru Rais kwa imani kubwa aliyoionyesha kwake kupitia uteuzi huo. Alisema uteuzi huo si tu ni heshima binafsi, bali ni wito wa kuwahudumia wananchi kwa moyo wa kujitolea, uadilifu na uwajibikaji wa hali ya juu.

“Kuteuliwa kwangu kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora ni heshima kubwa. Namshukuru sana Mhe. Rais kwa kuniamini. Naahidi sitawaangusha Watanzania na nitatumikia kwa kujitoa, kushirikiana na kuhakikisha kila mwananchi anahisi uwepo wa serikali,” alisema Wella kwa msisitizo.

Kabla ya uteuzi huu, Mhe. Wella alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, ambapo alionesha uwezo mkubwa wa kiutendaji, mshikamano wa kiutawala na usimamizi madhubuti wa shughuli za maendeleo. Uzoefu huu, alisema, unampa nguvu mpya ya kulihudumia vema eneo lake jipya la kiutawala.

Akizungumza mbele ya viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Tabora na wilaya zake, Wella alitoa shukrani kwa mapokezi mazuri aliyoyapata na kuahidi kushirikiana na kila mmoja katika kuhakikisha wilaya hiyo inasonga mbele. Alisisitiza kuwa mafanikio ya kweli hayaji kwa mtu mmoja, bali kupitia mshikamano na ushirikiano wa pamoja baina ya viongozi na wananchi.

“Nimepokelewa kwa upendo mkubwa na najua nina familia mpya hapa Tabora. Nitaendelea kushirikiana nanyi, kuwasikiliza na kufungua milango ya mawasiliano ili kwa pamoja tuhakikishe huduma zinawafikia wananchi kwa wakati, kwa haki na kwa ubora unaostahili,” alihitimisha.


 

PROF. CAROLYNE NOMBO ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA KAMPASI YA MZUMBE TANGA

July 03, 2025 Add Comment
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo ametembelea eneo la ujenzi wa Kampasi mpya ya Chuo iliyopo Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga, mnamo tarehe 2 Julai 2025 na kuridhishwa na kasi ya ujenzi huo. Ziara hiyo imelenga kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa kampasi hiyo ikiwa ni ufadhili wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET).

DKT.KIJAJI AZINDUA CHANJO YA MIFUGO NGORONGORO

July 03, 2025 Add Comment


Na Mwandishi Wetu, NCAA.


Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) amezindua zoezi la Chanjo ya Mifugo katika Kijiji cha Mokilal Tarafa ya Ngorongoro Mkoani Arusha ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa kitaifa wa miaka mitano wa kuchanja mifugo.

Dkt. Kijaji ameeleza kuwa katika utekelezaji wa zoezi hilo ambalo ni mpango wa kitaifa wa Miaka mitano kuanzia 2025-2030 ulizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 16 Juni, 2025 Bariadi Mkoani Simiyu na tayari kiasi cha shilingi bilioni 216 zimetengwa kufanya kazi hiyo na mwaka huu  zaidi ya Bilioni 62 imeshatolewa.

Amesema kuwa Serikali imetoa punguzo la bei na kila Ng'ombe mfugaji atachangia shilingi  500 badala ya  shilingi 1000 na Mbuzi na Kondoo wafugaji watachangia shilingi 300 pekee badala  ya shilingi 500 ambapo mpango huu unalenga kuwasaidia wafugaji.



Mkurugenzi wa huduma za Mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Benezeth Lutege ametaja 

Sababu za kuchanja mifugo hiyo kuwa ni

Kuongeza thamani mifugo kwenye masoko ya nje,  kujua idadi ya mifugo na wamiliki wake ili kurahisisha upangaji wa maeneo ya malisho na sababu nyingine kuwasaidia amana katika vyombo vya kifedha kupata mikopo kwa kuwa  taarifa za mifugo yao itakuwa inatambulika mifumo ya kielektroniki (barcode)  kupitia alama ya hereni za utambuzi kwa kila mmiliki wa mifugo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.  Kenan Kihongosi ameeleza kuwa Wananchi wa Ngorongoro na Mkoa wa Arusha kwa ujumla wamekuwa na muitikio mkubwa katika zoezi hilo na wataendelea kuhamasisha wafugaji wote kuchanja mifugo yao ili kutimiza azma ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuboresha maisha ya Wananchi

Mbunge wa Ngorongoro Mhe. Emmanuel Shangai ameishukuru Serikali kwa kuwasikiliza Wafugaji na kuwapatia chanjo ya mifugo yao na kuwaomba Wananchi wote kujitokeza kuchanja mifugo hiyo ili kuondokana na maradhi mbalimbali,  kuboresha afya na thamani ya mifugo yao.



REA YAJA NA MPANGO KABAMBE WA KUWEZESHA UJENZI WA VITUO VYA MAFUTA VIJIJINI

July 03, 2025 Add Comment
-Mkopo wa hadi Shilingi Milioni 133 kwa riba ya 5%-7% kutolewa

RAIS DKT SAMIA ANAPENDA KUFANYA KAZI NA VIONGOZI WA DINI-DKT BITEKO

July 03, 2025 Add Comment


📌 Asisitiza milango ya Rais Samia ipo wazi kwa ajili ya mazungumzo kwa mustakabali wa Taifa


📌 Asema Serikali inatambua na kuthamini kazi kubwa inayofanywa na Taasisi za dini


📌 Serikali kuendelea kushirikiana na Taasisi za dini kuchochea maendeleo


📌 Uchaguzi ni daraja la amani na maendeleo si chanzo cha mifarakano – Baba Askofu Shoo


📌 CCT yahimiza  maadili ya kisiasa, utulivu wa jamii na kampeni za kistaarabu


📌 Taasisi za dini Afrika zatajwa kuchangia maendeleo ya sekta ya afya kwa 30%- 70%


Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anapenda  kufanya kazi na viongozi wa dini kwa kuwa anawaongoza wananchi wenye dini ambao dini zao wanaziheshimu na hivyo asingependa kuona haki zao zinanyimwa kwa namna yoyote ile.

Dkt. Biteko amesema hayo Julai 3, 2025 jijini Dodoma wakati akimwakilisha  Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano Mkuu wa 32 wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT).

“Mheshimiwa Rais Samia anapenda kufanya kazi na viongozi wa dini na ninyi ni mashahidi amekuwa akiwaalika ili tuzungumze masuala mbalimbali ya kitaifa ingekuwa ni  mtu anayejifungia ndani na akasema analo jeshi, sheria, katiba na vyombo vya ulinzi basi nitafanya kazi nadhani hivi ingekuwa ngumu  sana lakini yeye amesema milango yetu iwe wazi tuzungumze na viongozi  wa dini kwa ajili ya kutafuta mustakabali wa nchi yetu pale ambapo  tunadhani hatuendi sawasawa,” amesema Dkt. Biteko. 

Akijibu hoja za CCT, Dkt. Biteko amesema kuwa imekuwa desturi ya nchi kuwa na waangalizi wa ndani kwenye Uchaguzi Mkuu na kuwa ni imani yake kuwa Tume Huru ya Uchaguzi  itawalika waangalizi wa ndani ikiwa ni pamoja na asasi za kiraia. Hata hivyo amesisitiza Tume Huru ya Uchaguzi iachiwe uhuru wake wa kufanya kazi zake. 

Amewahakikishia kuwa Serikali inatambua na kuthamini kazi kubwa inayofanywa na taasisi zote za dini ikiwemo makanisa na kusema kuwa tangu Uhuru mwaka 1961, Taasisi za dini zimeendelea kuchangia maendeleo ya kijamii na kiuchumi na kuwanufaisha watu wengi kote nchini. 

“Tunawapongeza sana na tunawashukuru sana kwa mchango wenu. Tafiti zinaonesha kuwa Taasisi za dini Barani Afrika huchangia kati ya asilimia30 hadi 70 ya maendeleo ya sekta ya afya. Kidunia, kwa mfano katika elimu, Vyuo kama University of Edinburgh - (Scotland), Oxford University - Uingereza na University of Kwa Zulu - Natal Afrika ya Kusini  vilianzishwa na Taasisi za dini,” amesema Dkt. Biteko.

Ameendelea kuzungumzia mchango wa taasisi za dini katika kuzalisha wataalamu wa fani mbalimbali duniani ambao wanaendelea kuiokoa dunia kutoka katika matatizo na majanga mbalimbali akitolea mfano  Tasisi ya World Coucil of Churches na World Vision kwa kutoa huduma za kibinadamu duniani kote bila kubagua tofauti zilizopo za dini, rangi, kabila na jinsia.

Katika kutambua mchango wa viongozi wa dini Afrika na duniani kote, Dkt. Biteko ameelezea haiba ya Mwanatheolojia Muanglikana kutoka Afrika Kusini, Hayati Baba Askofu Desmund MpiloTutu kama kiongozi wa dini mwenye upendo, mpendahaki na amani, ambaye amechangia kutetea haki za binadamu na kupambana dhidi ya u baguzi na hivyo kusaidia kuleta maendeleo na usawa kwa nchi ya Afrika Kusini na dunia kote.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikistro Tanzania, Baba Askofu, Dkt. Fredrick Shoo amepongeza usikivu wa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na juhudi za Serikali za kudumisha demokrasia kwa kuruhusu mikutano ya hadhara sambamba utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini.

Katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, Baba Askofu Dkt. Shoo amesema CCT inahimiza maadili ya kisiasa na utulivu wa jamii ikiwa ni pamoja na kampeni zisizo za kuvunjiana heshima bali zinazoweka mbele maslahi ya Taifa na kupinga vitendo vyote vya rushwa.

“ Uchaguzi ni daraja la amani na maendeleo si chanzo cha mifarakano, jamii idumishe amani, mshikamano na uzalendo wa kila mmoja kwa nafasi yake. Pia Tume Huru ya Uchaguzi iendelee kusimamia haki kwa kushirikiana na waangalizi wa ndani amesema ,” Baba Askofu Shoo.


Amebainisha kuwa CCT itaendelea kushirikiana na Serikali kuleta maendeleo ya jamii hivyo ameiomba Serikali itoe unafuu wa kodi na kutotoza ruzuku kwa misaada inayotolewa na wahisahi ili kuboresha ubora wa huduma na kuwafikia wananchi.

Katibu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Mchungaji Dkt. Moses Matonya amesema kuwa CCT ni Jumuiya inayounganisha  madhehebu wanachama 12 na mashirika ya kikristo 14. Aidha katika Mkutano huo jumla ya  wajumbe waliohudhuria ni  224 kati ya wajumbe wote 280.



Mwisho

EWURA YAENDELEA KUTOA ELIMU KWENYE MAONESHO SABASABA

July 02, 2025 Add Comment
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu majukumu yake na namna ya kushiriki katika ufuatiliaji wa huduma za nishati na maji nchini, kupitia ushiriki wake kwenye Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere.

WMA Yatoa Onyo Kali kwa Wafanyabiashara Wahujumu Vipimo vya Mafuta

July 02, 2025 Add Comment
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

MENEJA wa Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) Kitengo cha Bandari, Alfred Shungu amesema kuwa wafanyabiashara wanaobainika kuhujumu vipimo vya mafuta, hasa kwa kutumia vifaa visivyotimiza viwango, watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kifungo au faini isiyozidi Shilingi Milioni 20 kwa kosa la kwanza.

MTENDAJI MKUU ADEM ASISITIZA UMUHIMU WA MAAFISA ELIMU KATA NCHINI KUJENGEWA UWEZO KUHUSU USIMAMIZI WA SHUGHULI ZA ELIMU

July 02, 2025 Add Comment
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), Dkt. Maulid J. Maulid, ameeleza Maafisa Elimu Kata wanawajibika kusimamia shughuli za elimu kwenye ngazi ya Kata, hivyo ni muhimu Maafisa hao kujengewa uwezo kuhusu usimamizi fanisi wa shughuli za elimu ili kuchagiza maendeleo ya sekta ya elimu katika ngazi ya Kata.

REA na Oryx Gas Waanzisha Mradi wa Nishati Safi kwa Magereza Simiyu

July 01, 2025 Add Comment
Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Oryx Gas kwa kushirikiana na Wakala wa Nishati Safi Tanzania (REA) wamezindua rasmi mradi mkubwa ambao utawafikia na kuwawezesha wafanyakazi wote wa Magereza kuacha matumizi ya mkaa na kuni na kuhamia matumizi ya gesi.

Benki ya CRDB yaandika historia kuorodhesha Kijani Bond Soko la Hisa Luxembourg

July 01, 2025 Add Comment

 

Luxembourg, 1 Julai 2025 – Benki ya CRDB imeweka historia kwa kuorodhesha rasmi hatifungani yake ya kwanza ya kijani maarufu kama ‘Kijani Bond’ katika Soko la Hisa la Luxembourg (LuxSE). Hatua hii inaifanya Benki ya CRDB kuwa miongoni mwa benki za kwanza za biashara Kusini mwa Jangwa la Sahara kuorodhesha hatifungani ya kijani iliyotolewa nchini katika soko hilo la kimataifa na pia kuonekana katika Soko la Hisa la Kijani la Luxembourg (LGX), jukwaa linaloongoza duniani kwa masuala ya fedha endelevu.

Kijani Bond ilizinduliwa kwa mafanikio nchini Tanzania ikivutia wawekezaji wengi na kukusanya zaidi kwa thamani ya Shilingi Bilioni 171.8 (sawa na Dola za Marekani Milioni 65.7). Kuorodheshwa kwake katika orodha rasmi ya Dhamana za Soko la Hisa la Luxembourg (LuxSE SOL) ni ushuhuda wa kuongezeka kwa mahitaji na uwezo wa Afrika kuwekeza katika miradi ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi huku ikivutia masoko ya mitaji ya kimataifa.

Hafala ya kuorodheshwa kwa hatifungani hiyo imefanyika katika kwenye makao makuu ya LuxSE, ikihudhuriwa na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji na Luxembourg, Bw. Juma Ali Salum, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Mussa Nsekela, Afisa Mkuu wa Biashara na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya LuxSE, Arnaud Delestienne, pamoja na viongozi wengine waandamizi kutoka Benki ya CRDB, LuxSE na Orbit Securities Tanzania mawakala wa uuzaji wa dhamana hiyo ambayo pia imeorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, alisema: “Kuorodheshwa kwa Kijani Bond si tu hitimisho la mchakato wa kifedha, bali ni mwanzo wa ushirikiano mpya kati ya Afrika na Ulaya katika kufadhili uchumi wa kijani. Tuna fahari kuwa waanzilishi katika nyanja hii kwa kufanikisha ukusanyaji wa zaidi ya Dola Milioni 65.7 kupitia dhamana yetu ya kwanza ya kijani, ambayo ilispata mafanikio ya zaidi ya asilimia 429. Leo, tunaipeleka safari yetu ya uendelevu katika jukwaa la kimataifa, si kwa ajili ya kupata fedha pekee, bali pia kuinua viwango vyetu vya ufadhili endelevu. Huu ni ujumbe kwa dunia: Afrika ipo tayari kuongoza katika ufadhili endelevu kwa ubunifu, uadilifu, na dhamira ya kweli.”

Kijani Bond ni hatifungani ya kwanza ya aina yake nchini Tanzania na miongoni mwa kubwa zaidi Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa wakati wa kutolewa. Fedha zilizopatikana kupitia dhamana hii tayari zinaelekezwa katika sekta mbalimbali zenye mchango mkubwa kwa maendeleo endelevu ikiwemo: Nishati mbadala, Kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi, Nishati safi ya kupikia, Majengo rafiki kwa mazingira, Usafiri wa kijani, Maji safi na huduma bora za usafi wa mazingira, pamoja na miradi mingine inayozingatia mabadiliko ya tabia nchi.

Kwa upande wake, Arnaud Delestienne, Afisa Mkuu wa Biashara wa LuxSE, alisema: “Tunafurahia kuikaribisha Benki ya CRDB na hatifungani yake ya kijani katika soko letu. Huu ni ushahidi wa namna masoko ya mitaji ya kimataifa yanavyoweza kusaidia kupata fedha kwa ajili ya huduma muhimu na kuchochea mabadiliko ya kijani barani Afrika. Pia ni uthibitisho wa nafasi ya Afrika kama mshirika muhimu katika maendeleo ya fedha endelevu duniani.”

Akitoa salamu kutoka kwa Serikali ya Tanzania, Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji na Luxembourg, Juma Ali Salum, alieleza:

“Tukio hili ni la kujivunia kwa taifa letu na ni kielelezo cha dhamira ya Tanzania katika kushiriki kikamilifu katika ajenda ya kimataifa ya mabadiliko ya tabianchi chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Kijani Bond ya Benki ya CRDB inaonyesha dhamira ya nchi yetu kuwa mfano wa maendeleo jumuishi na yanayozingatia mabadiliko ya tabianchi.”

Benki ya CRDB ikiwa ni taasisi iliyoidhinishwa na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (UN-GCF), inaendelea kujijengea nafasi thabiti kama kiongozi wa ufadhili endelevu katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. Kuorodheshwa kwa Kijani Bond katika Soko la Hisa la Luxembourg kunaiwezesha benki kupanua wigo wake wa kupata mitaji ya kimataifa huku ikiimarisha mchango wake katika kusaidia jitihada za serikali kukuza uchumi wa kijani.
Kupitia dhamana hiyo, Benki ya CRDB tayari imefanikiwa kuwezesha maelfu ya wanawake na vijana kuanzisha na kukuza biashara zao, kusaidia wakulima kutumia mbinu za kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi, pamoja na kuboresha maisha ya watu katika jamii mbalimbali nchini Tanzania Kwa taarifa zaidi kuhusu Dhamana ya Kijani ya CRDB Bank, tafadhali tembelea: 🔗 https://www.luxse.com/security/TZ1996105155/416649