NEEC WAJA NA FURSA ZA KIUCHUMI KATIKA MAONEHO YA 49 YA KIMATAIFA YA BIASHARA (SABA SABA)
habariMRADI WA BOMBA LA GESI NTORYA–MADIMBA KUGHARIMU SHILINGI BILIONI 120
habariTBS YAWASILISHA UTEKELEZAJI WA SERA YA KURUDISHA KWA JAMII
habariNAIBU WAZIRI UMMY AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUGHARAMIA MAZISHI WALIOFARIKI SAME
habariNa Mwandishi Wetu - KILIMANJARO
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa moyo wake wa upendo kwa kugharamia mazishi ya miili 42 ya watu waliofariki dunia kufuatia ajali iliyotokea Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.
Mhe. Nderiananga ametoa shukrani hizo tarehe 03 Julai, 2025 wakati aliposhiriki tukio la kuaga miili 35 katika viwanja vya Hospitali ya Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC) akisema miili Saba ilichukuliwa na ndugu zao na miili miwili bado vipimo vya DNA vinafanyiwa kazi ili kutambulika.
![]() |
Tukio hilo lilioongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Nurdin Babu ambapo Mhe. Nderiananga alimpongeza kwa kujitoa kwa kiasi kikubwa tangu ilipotokea ajali hiyo akishirikiana na watendaji wake wote.
![]() |
Amesema Serikali kupitia Idara ya Menejimenti ya Maafa iliyopo Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Kilimanjaro kwa juhudi kubwa zilizofanyika kuokoa manusura wa ajali hiyo pamoja na miili ya walioungua kwa moto mara baada ya ajali kutokea.
Vilevile ameipongeza Serikali kupitia Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kuchukua sampuli za miili hiyo (DNA) kuhakikisha ndugu wanatambua miili ya wapendwa wao.
Hata hivyo Mhe. Nderiananga ameendelea kutoa pole kwa Serikali, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia msiba huo mzito kwa Taifa huku akiwaomba kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu hadi watakapokamilisha kuwahifadhi wapendwa wao.
Aidha, ajali hiyo iliyotokea Juni 28 2025 katika Kitongoji Mahuu, Kata ya Same, takribani kilomita nne kutoka Same mjini, ililihusisha basi kubwa la abiria, Mali ya Kampuni ya Chanel One, lenye namba za usajili T 179 CWL na basi dogo la abiria aina ya Toyota Coaster, lenye namba T 199 EFX linalomilikiwa na Kampuni ya Mwami Trans.
Coaster hiyo, ilikuwa ikitokea Same kuelekea Manispaa ya Moshi, wakati basi la Chanel One lilikuwa likitokea Arusha kuelekea Tanga.
PROF. CAROLYNE NOMBO ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA KAMPASI YA MZUMBE TANGA
habariREA YAJA NA MPANGO KABAMBE WA KUWEZESHA UJENZI WA VITUO VYA MAFUTA VIJIJINI
habariEWURA YAENDELEA KUTOA ELIMU KWENYE MAONESHO SABASABA
habariWMA Yatoa Onyo Kali kwa Wafanyabiashara Wahujumu Vipimo vya Mafuta
habariMTENDAJI MKUU ADEM ASISITIZA UMUHIMU WA MAAFISA ELIMU KATA NCHINI KUJENGEWA UWEZO KUHUSU USIMAMIZI WA SHUGHULI ZA ELIMU
habariREA na Oryx Gas Waanzisha Mradi wa Nishati Safi kwa Magereza Simiyu
habariSubira Mgalu Aonyesha Nia ya Kuliongoza Jimbo la Bagamoyo
habariMWENYEKITI TUGHE MKOA WA DAR ES SALAAM AJITOSA MBIO ZA UBUNGE KIVULE
habariHali ya joto la kisiasa katika mtanange wa mbio za Ubunge katika Jimbo jipya la Kivule Mkoani Dear es Salaam, imeanza kupanda, baada ya Mjumbe wa Kamati Kuu Taifa ya Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) *Komredi Brendan Maro, pichani kulia ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, kujitosa kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge katika Jimbo hilo jipya.
Komredi Maro anakumbukwa kwa jitihada zake za kuwaunganisha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (Umma na Sekta Binafsi) Katika kutekeleza wajibu wao kwa waajiri, lakini pia katika kujenga hoja za kulindwa kwa Utu, haki na maslahi ya wafanyakazi. Pamoja na nafasi hizo, Komredi Maro amewahi kuhudumu pia kama Mwenyekiti wa Mkoa wa Shirisho la Vyama huru vya Wafanyakazi (TUCTA) Mkoa wa Dar es Salaam, ambako anakumbukwa kwa kushiriki kikamilifu Katika hoja za maboresho ya Sheria na Kanuni za mafao (Kikotoo), huku akifanikiwa kuwaunganisha na kuwashawishi Wafanyakazi kuendelea kuwa watulivu na kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi, akiwahakikishia TUCTA inaendelea na majadiliano na Serikali Katika kutafuta mwafaka.
Hivi Karibuni, kupitia Sherehe za MeiMosi, Mhe.Rais *Dkt. Samia Suluhu Hassan,* alitangaza maboresho ya Kanuni hiyo na kupandisha kima cha chini cha mshahara na nyongeza ya mshahara kwa Watumishi wa Umma, kama matokeo ya majadiliano baina ya Serikali na TUCTA.
Komredi Maro, ambaye ni Mkazi wa Kata ya Kitunda, Jimboni Kivule, anatajwa kuwa mmoja kati ya vijana wasomi waliolelewa katika Chama cha Mapinduzi, aliyeshiriki katika kampeni mbalimbali za chama, wenye upeo na uwezo wa uchambuzi, kujenga hoja na kutoa ushawishi kwa watu, sifa zinazopelekea aonekane kuwa mmoja wa watu sahihi sana kwa changamoto za Jimbo la Kivule.
Aidha, kawaida yake ya ushirikiano siyo tu na viongozi wenzake lakini pia na watu anaowaongoza inatajwa kuwa turufu muhimu kwake Katinka mbio hizo.
Hata hivyo, licha ya uwezo wake wa kuimudu nafasi hiyo, changamoto inayoweza kumkabili ni kuwa mtu aliyetokea kwenye Familia ya kawaida kabisa kiuchumi, hali inayoweza kukwamisha mpambano wake mbele ya watia nia wenye uchumi mkubwa.
Juhudi za kumpata ili kuelezea jinsi alivyojiandaa na mpambano huu hazikuzaa matunda, baada ya kujibu kwa ufupi kuwa "Chama chetu na Wanakivule wenyewe wanakijua wanachokitaka na namna ya kukipata."
KANISA LA ANGLIKANA DAYOSISI YA DAR YAANDAA BONANZA KUCHANGIA UJENZI WA JENGO LA KITEGA UCHUMI
habariWATUMISHI WA MAGEREZA MANYARA WAPATIWA MAJIKO YA GESI
habari📌Mifumo ya uzalishaji wa bayogesi 126 mbioni kuanza
📌REA, Jeshi la Magereza kununua mashine 61 za mkaa mbadala
📌REA kuwajengea uwezo magereza uendelezaji miradi ya nishati safi
📌Mha. Saidy amewataka magereza kuwa mabalozi wa nishati safi
Serikali imewapatia watumishi wa Jeshi la Magereza mitungi ya gesi na majiko ya gesi ya kupikia ili kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa watumishi na wananchi iliyolenga kufikia malengo yaliyoainishwa kwenye mkakati wa kitaifa wa matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini.
Hayo yamebaibishwa leo Juni 26, 2025 na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhe. Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu wakati wa uzinduzi wa kugawa majiko ya gesi kwa watumishi wa magereza iliyofanyika gereza la Babati mkoani Manyara.
Amesema kuwa, katika mkoa wa Manyara tayari Serikali imegawa mitungi ya gesi na majiko ya gesi yapatayo 330 kwa watumishi wa jeshi la magereza na katika gereza la Babati jumla ya majiko na mitungi 150 wamegawiwa watumishi hao wa magereza.
Amesema kuwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeingia makubaliano na Jeshi la Magereza ya kuwawezesha magereza kuhama kutoka katika matumizi ya nishati isiyo salama kwenda katika matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia katika magereza yote nchini.
"Kuanzia mwanzoni wa mwezi januari 2025 jeshi la magereza walishaingia kwenye matumizi ya nishati safi na salama na tayari wameachana na nishati isiyo salama na chafu kwa afya na mbaya kwa mazingira yetu, " Ameongeza.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mha. Hassan Saidy amewataka watumishi wa jeshi la magereza kuibeba ajenda ya Mhe. Rais Samia ya kuwa mabalozi wa nishati safi ya kupikia hapa nchini.
![]() |
Katika hatua nyingine Mha. Saidy ameeleza kuwa, mifumo ya uzalishaji wa bayogesi ipatayo 126 tayari ipo mbioni kuanza kwa kushirikiana na jeshi la magereza ambayo itawezesha ununuzi wa mashine za kutengeneza mkaa mbadala 61, vile vile kuwajengea uwezo watumishi wa jeshi la magereza ya kuendeleza miradi hiyo ya nishati.
Kwa upande wake, Mkuu wa Magereza mkoa wa Manyara ACP Solomon Mwambingu amemshukuru Rais Samia kwa kuwapatia watumishi wa magereza majiko ya gesi na mitungi ya gesi na kusisitiza kuwa wataendelea kuwa mabalozi wa nishati safi ya kupikia katika jamii yote inayowazunguka.
SERIKALI YAWAREJESHA WATANZANIA 42 KUTOKA NCHINI IRAN NA ISRAEL.
habariNIDHAMU, UWAJIBIKAJI CHACHU YA MAFANIKIO KATIKA SEKTA YA ELIMU: MTENDAJI MKUU ADEM
habariMafunzo hayo yamelenga kuwawezesha Maafisa Elimu Kata kusimamia kwa ufanisi shughuli zote za elimu katika ngazi ya Kata.
Dkt. Maulid J. Maulid amesema Maafisa Elimu Kata wana wajibu wa kutambua na kutafsiri kwa vitendo maono ya Serikali kwa kuhakikisha wanakuwa wasimamizi wa kwanza wa maboresho makubwa yaliyofanyika katika sekta ya elimu kwa kuboresha Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014 Toleo la 2023 na Mtaala ulioboreshwa ili kufikia lengo la Serikali la kuboresha na kuimarisha sekta ya elimu nchini.
“Mabadiliko na mageuzi yanayotegemewa kutokea kwa utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mtaala ulioboreshwa yako kwenye meza zenu kama wasimamizi wa kwanza wa shughuli za elimu katika ngazi ya Kata. Tunawaomba mwende mkasimamie ipasavyo mageuzi hayo na tuone matokeo kuanzia kwenye ngazi ya Shule na Kata kwa kwenda kutekeleza kwa vitendo yale mtakayojifunza kwenye mafuzo haya kwani hayo ndio yatakuwa dira ya kuwasaidia kufanya usimamizi fanisi wa shughuli zote za elimu katika ngazi ya Kata na hatimaye lengo la Serikali kufikiwa”. Amesema Dkt. Maulid.
Aidha, Dkt. Maulid amesisitiza Maafisa Elimu Kata hao kuitambua, kusoma, kuelewa na kutekeleza miongozo yote inayotolewa na Mamlaka zinazosimamia elimu nchini ikiwa ni pamoja na Ofisi ya Kamishna wa elimu ili iwasaidie katika utekelezaji wa majukumu yao ya usimamizi wa shughuli za elimu kwenye ngazi ya Kata kwa ufanisi.
Vilevile Dkt. Maulid amesisitiza usimamizi wa nidhamu, uwajibikaji, ufundishaji na ujifunzaji mahiri wenye kuinua ubora wa elimu inayotolewa shuleni.
Nae Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma Dkt. Alphonce J. Amuli amesema washiriki wa mafunzo hayo watajengewa uwezo katika maeneo ya Uongozi, Usimamizi na Utawala katika Elimu, Utawala Bora katika Elimu, Uandaaji wa Mpango wa Jumla wa Maendeleo ya Elimu Ngazi ya Serikali za Mitaa, Ufuatiliaji na Usimamizi Fanisi wa Shule, Usimamizi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Shule, Ukaguzi wa Ndani, na Ushirikishwaji wa Jamii na Utatuzi wa Malalamiko katika Elimu. Dkt. Amuli pia amesema kuwa ni dhahiri kwamba, maeneo hayo yatakayowezeshwa yatasaidia kuimarisha usimamizi na uendeshaji wa shule kwa ufanisi.
Mafunzo ya Utawala Bora wa Elimu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa yanafanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 25 – 27 Juni, 2025 ADEM Bagamoyo na yamefadhiliwa na mradi wa BOOST chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia


TANZANIA KUTOATHIRIKA MOJA KWA MOJA NA UMOJA WA BRICS.
habari
Na. Saidina Msangi, WF, Dodoma.
Serikali imesema kuwa Tanzania haitapata athari za moja kwa moja kutokana na mafanikio au changamoto zozote katika Umoja wa BRICS (Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini), zinazoweza kutokea katika sekta ya kiuchumi na fedha hususani ya kujiondoa kwenye Dolarisation kwa kuwa sio nchi mwanachama wa BRICS.
Hayo yalisemwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), alipokuwa akijibu swali la Mheshimiwa Zahor Mohammed Haji (Mwera), aliyeuliza faida na hasara ya Tanzania kutokana na msimamo wa nchi za BRICS ambazo zimejipanga kujiondoa kwenye mfumo wa Dolarisation.
Alisema Serikali ya Tanzania imekuwa na ushirikiano wa muda mrefu na nchi za BRICS (Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini) katika nyanja mbalimbali ikijumuisha masuala ya kiuchumi, biashara na diplomasia kwa kuendelea kuwepo kwa balozi za nchi hizo hapa nchini na Tanzania kuwa na balozi katika nchi hizo.
’’Kwa sasa Tanzania sio mwanachama wa BRICS ila inashiriki katika mikutano ya BRICS kama observer, hivyo mafanikio au changamoto zozote katika umoja huo zinazoweza kutokea katika sekta ya kiuchumi na fedha hususani ya kujiondoa kwenye Dolarisation, hatutakuwa na athari za moja kwa moja kwa kuwa sio wanachama wa BRICS,’’ alifafanua Mhe. Chande.
Mhe. Chande alisema mahusiano ya Tanzania na nchi hizo yanadumishwa kwa kuendelea kuwepo kwa balozi za nchi hizo hapa nchini na Tanzania kuwa na balozi katika nchi hizo.
Aliongeza kuwa mahusiano hayo yanaendelea kuleta mafanikio chanya kwa Serikali ya Tanzania kwa kutumia fursa za kiuchumi zinazopatikana katika nchi hizo ambazo pia zinaimarisha mahusiano ya uwili baina yake (bilateral engagement).