MIRADI YA CSR YA BARRICK BULYANHULU YAENDELEA KUBORESHA MAISHA WANANCHI NYANG’HWALE

November 04, 2026

 

Muonekano wa nyumba ya watumishi katika Zahanati ya Iyenze, Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale, Mkoa wa Geita.

Muonekano wa Shule Mpya ya Msingi Sengerema iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale, Mkoa wa Geita.

 Muonekano wa Shule ya Msingi Kharumwa English Medium iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale, Mkoa wa Geita.

Muonekano wa matundu ya vyoo katika Shule ya Sekondari Nyang’hwale, Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale, Mkoa wa Geita, ikiwa ni sehemu ya miradi ya kuboresha miundombinu ya elimu kupitia fedha za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) za Mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
Muonekano wa madarasa katika Shule ya Sekondari Nyang’hwale, Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale, Mkoa wa Geita.
Jengo la Soko la Madini la Nyang’hwale, Mkoa wa Geita, likiwa katika hatua za mwisho za ujenzi kupitia mradi unaofadhiliwa kwa fedha za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) zilizotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale, John Isaac (mwenye kofia ya bluu), akiongoza wajumbe wa kamati yake kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwa fedha za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) zilizotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu.

**
Mgodi wa Barrick Bulyanhulu uliopo katika Halmashauri ya wilayani Msalala, Mkoani Shinyanga, unaendelea kuleta manufaa kwa wananchi kutokana na kuwa kinara wa kutekeleza sera na kanuni ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) ambapo umefanikisha miradi mikubwa ya maendeleo ambayo imeboresha maisha ya wananchi wengi wanaoishi maeneo yanayozunguka mgodi huo.

Miradi mikubwa iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa ipo kwenye sekta za elimu, afya, maji, uwezeshaji wa wananchi kiuchumi na ujenzi wa miundombinu ya barabara.

Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha , Utawala na Mipango katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale John Isaac akiongea katika ziara ya kamati yake kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwa fedha za CSR katika kata za Karumwa kafita na Izunya alisema uwepo wa mgodi wa Bulyanhulu unazidi kuchangia na kuchochea maendeleo katika halmashauri hiyo kutokana na kufanikisha miradi ya kuboresha maisha ya wananchi.

Katika ziara hiyo kamati pia ilitembelea mradi mpya wa Soko jipya la dhahabu linalojengwa katika Halmashauri kwa fedha za CSR ambalo litarahisisha biashara ya madini katika halmashauri hiyo na kufanikisha kuongeza mapato ya serikali kupitia tasnia ya madini na kuwa chanzo cha ukuaji wa uchumi kwa wachimbaji wadogo
Kamati hiyo imeridhishwa na utekelezaji wa miradi iliyopangwa kukamilika kwa mwaka huu ambayo iko mbio kuikamilika tayari kwa kuanza kutumiwa na wananchi kuanzia mwaka ujao.

Katika kipindi cha mwaka huu, Barrick ilisaini mkataba wa kutoa fedha za CSR kiasi cha shilingi milioni 900 kwa ajili ya kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo yenye lengo ya kuboresha maisha ya wananchi.

Baadhi ya miradi inayotekelezwa katika kipindi cha mwaka huu ni ujenzi wa soko la dhahabu (awamu ya kwanza), ufugaji wa nyuki katika msitu wa Miyenze, ujenzi wa nyumba ya mtumishi na uchimbaji wa kisima katika shule ya sekondari Iyenze pamoja na ununuzi wa vitanda 240 kwa mabweni ya shule za sekodari za Bukwimba, Busolwa na Kenegele.

Aidha, miradi mingine ni pamoja na ununuzi wa madawati na samani za walimu katika Shule Mpya ya Msingi Sengerema, ukamilishaji wa miundombinu ya maji na umeme katika Zahanati ya Mwabui, ununuzi wa vifaa vya TEHAMA kwa watendaji wa vijiji na kata ya Mwingiro, pamoja na uchimbaji wa rambo la kunyweshea mifugo katika kijiji cha Ng’wasabuka.

Katika kipindi cha mwaka uliopita mgodi wa Barrick Bulyanhulu ulitoa kiasi cha shilingi bilioni 1 na milioni 75 za uwajibikaji kwa jamii (CSR) ambazo zimefanikisha miradi mbalimbali ya kijamii ya kuboresha maisha ya wananchi.

Wananchi wanaoishi katika maeneo ya miradi katika halmashauri za Wilaya ya Nyang’hwale, wameshukuru Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa kufanikisha miradi mikubwa kupitia fedha za CSR.

 Miradi hiyo ambayo inaendelea kuyafanya maisha yao kuwa bora itadumu kwa muda mrefu, pia itanufaisha vizazi vijavyo hata baada ya kufungwa kwa shughuli za mgodi.

Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »