Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo CPA. Ashraph Abdulkarim amewashauri wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo kutangaza bidhaa zao mtandaoni jambo litakaloendelea kutavutia wateja wengi zaidi wa ndani na nje ya nchi.
Ushauri huo umetolewa wakati wa mkutano baina ya uongozi wa shirika hilo na wafanyabiahara wa Soko soko hilo, mkutano ambao umelenga kusikiliza kero na changamoto za wafanyabiashara ili kuendelea kuboresha mazingira ya biashara katika soko hilo.
Amebainisha kuwa shirika limeendelea na mipango mbalimbali ya kuvutia wateja kwa kutangaza huduma na bidhaa zinazopatikana sokoni hapo, jitihada ambazo zimekuwa na mafanikio chanya kwa kuongeza mzunguko wa watu wanakuja na kutoka sokoni hapo.
Ameongeza kuwa kutokana na mabadiliko ya teknolojia nchni, ubunifu katika kuendesha biashara ni jambo lisiloepukika, kwakuwa mtu anaweza kufanya maamuzi ya bidhaa anayoitaka akiwa nyumbani au mahali popote na kuja kuichukua au kutuma mtu aifuate kwa niaba yake.
Shirika la Masoko ya Kariakoo limekuwa na utaratibu wa kukutana na wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo kila baada ya miezi mitatu kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili, kupokea mrejesho na kushirikisha shughuli mbalimbali zinazoendelea sokoni hapo ili kujenga uelewa wa pamoja miongoni mwao.





EmoticonEmoticon