
Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera, amekabidhi magari mawili gari la zimamoto na gari la TANESCO kwa wananchi wa Jimbo la Namtumbo, mkoani Ruvuma, ili kuboresha huduma za kijamii na kiufundi kwa wananchi wa eneo hilo.
Akizungumza katika Site Trust Nishati Safi Marathoni 2026 leo, Octoba 24, 2026 Wilayani Namtumbo, Dkt. Homera amesema awali wananchi walipokumbwa na majanga ya moto walilazimika kupata haduma ya Zimamoto toka Songea hivyo Kupatikana kwa gari la zimamoto kutarahisisha huduma hiyo na kuisogeza karibu na wananchi.

Aidha, ameeleza kuwa wananchi wa Lusewa walikuwa walisafiri zaidi ya kilomita 100 kufuata huduma za kiufundi za TANESCO, hivyo kupatikana kwa gari la TANESCO sasa kutawawezesha wananchi kupata huduma hizo kwa haraka na kwa ukaribu zaidi.
Dkt. Homera amezitaja kata zitakazonufaika moja kwa moja na huduma za kiufundi kwa kupitia gari la TANESCO kuwa ni Magazini, Msisima, Lusewa, Lijela na Kaole, pamoja na maeneo jirani.
EmoticonEmoticon