WAZIRI DKT.HOMERA AWASILISHA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA NISHATI KWA ROBO YA KWANZA YA MWAKA WA FEDHA 2026/2027

October 19, 2026

Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera, amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya Wizara ya Nishati kwa kipindi cha Julai hadi Septemba 2026 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti, Mhe. Simon Songe (Mb), leo Oktoba 19, 2026.

Kikao hicho kimehudhuriwa na wajumbe wa Kamati hiyo, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba (Mb), Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Umeme na Nishati Jadidifu, Mha. Felchesmi Mramba, Katibu Mkuu anayeshughulikia Mafuta na Gesi Asilia, Dkt. James Mataragio, Menejimenti ya Wizara, Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati pamoja na baadhi ya wajumbe wa menejimenti za taasisi hizo.





Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »