TANZANIA KUTAFUTA SHILINGI TRILIONI 7.3 MKUTANO WA COP 31

October 27, 2026
Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Kemilembe Mutasa akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Dkt. Richard Muyungi wakati wa ufunguzi wa kikao cha Wataalamu kilichofanyika tarehe 27, Oktoba 2026 Jijini Dar es Salaam kujadili maandalizi ya Tanzania kuelekea Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama Wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP 31).

******************

WATAALAMU wamehimizwa kuandaa mapendezo na msimamo mahsusi ya Tanzania katika Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP 31) ili kuwezesha upatikanaji wa Shilingi trilioni 7.3 za miradi ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi.

Hayo yamesema Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi katika hotuba yake iliyosomwa na Mkurugenzi wa Mazingira, Kemilembe Mutasa wakati wa ufunguzi wa kikao cha Wataalamu kilichojadili maandalizi ya Tanzania kuelekea Mkutano wa COP 31 unaotarajia kufanyika Antalya, Uturuki tarehe 9-20 Novemba mwaka huu.

Dkt. Muyungi amesema mkutano huo ni jukwaa mahsusi la kuiwezesha Tanzania kupata fedha za za miradi ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi hususani katika kipindi hiki cha utekelezaji wa Dira ya taifa ya maendeleo 2050.

“Programu ya mageuzi ya usimamizi wa mazingira kuelekea dira 2050 imeanisha mahitaji ya kiasi cha shilingi trilioni 7.3…kuelekea katika mkutano huo ni wajibu wetu tutahakikisha fedha hizi zinapatikana kupitia majadiliano katika mkutano huo” amesema Dkt. Muyungi.

Ameeleza kuwa wadau wanaoshiriki mkutano huo kutoka Tanzania, hawana budi kuweka mbele maslahi ya Watanzania Milioni 60 kwa kupaza sauti zao kwa pamoja kwani kwa kufanya hivyo kutaimarisha utambulisho na uwakilishi wao.

Amesema katika mkutano wa COP 30 uliofanyika nchini Brazil, Tanzania ilikuwa Mwenyekiti wa Kundi la Afrika la Majadiliano kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (AGN) ambapo iliweza kuratibu msimamo wa pamoja wa Afrika ikiwemo upatikanaji wa fedha za tabianchi na utekelezaji wa makubaliano ya kimataifa.

Ametaja baadhi ya mafanikio iliyopata Tanzania katika Mkutano COP 30 ni pamoja uanzishwaji wa kituo cha mafunzo ya majadiliano ya tabianchi kwa vijana, ambapo hivi karibuni Ofisi ya Makamu wa Rais iliratibu mafunzo ya kwanza yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam tarehe 20-22 Oktoba mwaka huu.

Amefafanua kuwa mafanikio mengine yaliyopatikana ni kuandaliwa na kuzinduliwa kwa kitabu cha kumbukumbu cha Miaka 30 ya AGN, ambapo kitabu hicho kimeweka kumbukumbu ya historia, mafanikio, changamoto na mchango wake katika majadiliano na maamuzi ya kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi.

Dkt. Muyungi amesema mkutano huo pia uliwezesha kuanzishwa kwa ofisi ya kikanda ya mtandao wa Santiago ikiwa ni hatua muhimu katika kuimarisha upatikanaji wa msaada wa kiufundi kwa nchi za Bara la Afrika.

Kwa upande Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Bahari kutoka Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi, Zanzibar, Dk. Makame Omar Makame amesema Zanzibar ni moja ya maeneo yaliyopo hatarini kukabiliwa na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi kupitia sekta za uzalishaji mali ikiwemo kilimo, uvuvi n.k.

Amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inatarajia kushiriki katika Mkutano wa COP 31 kuunganisha nguvu za pamoja na kuweka mkazo na msisitizo katika upatikanaji wa fedha za miradi ya uhifadhi wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi.

“Fedha zitakazopatikana zitawezesha kujenga kuta za kuzuia mmomonyoko katika fukwe za bahari na uingiaji wa maji ya chumvi na pia kusaidia utoaji wa elimu kuhusu masuala ya mabadiliko ya tabianchi kwa jamii” amesema Dkt. Makame.

Mwakilishi kutoka Shirika la Shirika la kimataifa la uhifadhi wa mazingira na maendeleo endelevu (IUCN), Bw. Ghaamid Abdulbasat amesema Shirika hilo limeendelea kuimarisha ushirikiano na Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais katika utekelezaji wa ahadi za mikataba ya kimataifa ya mabadiliko ya tabianchi.

Akitolea mfano amesema Shirika hilo kwa linashirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais inatekeleza Programu ya Urejeshaji ya kidunia (TRI) inayolenga kurejesha uoto wa asili katika ardhi iliyoharibika takribani hekta milioni 5.2 ifikapo mwaka 2030 katika mabonde ya Ruaha Mkuu na Ziwa Rukwa, katika mikoa ya Iringa, Mbeya na Rukwa.

Wataalamu kutoka taasisi za umma, sekta binafsi na wadau wa maendeleo wakifuatilia kikao cha wataalamu kilichofanyika tarehe 27, Oktoba 2026 Jijini Dar es Salaam kujadili maandalizi ya Tanzania kuelekea Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama Wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP 31).
Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira na maendeleo endelevu (IUCN), Bw. Ghaamid Abdulbasat akizungumza wakati wa kikao cha wataalamu kilichofanyika tarehe 27, Oktoba 2026 Jijini Dar es Salaam kujadili maandalizi ya Tanzania kuelekea Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama Wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP 31).
Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Thomas Chali Makame akizungumza wakati wa kikao cha wataalamu kilichofanyika tarehe 27, Oktoba 2026 Jijini Dar es Salaam kujadili maandalizi ya Tanzania kuelekea Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama Wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP 31)
Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Bahari kutoka Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi, Zanzibar, Dk. Makame Omar Makame akizungumza wakati wa kikao cha wataalamu kilichofanyika tarehe 27, Oktoba 2026 Jijini Dar es Salaam kujadili kuhusu maandalizi ya Tanzania kuelekea Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama Wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP 31)
Wataalamu kutoka kutoka taasisi za umma, sekta binafsi na wadau wa maendeleo wakijadiliana masuala mbalimbali muda mfupi baada ya ufunguzi wa kikao cha wataalamu kilichofanyika Oktoba 27, 2026 Jijini Dar es Salaam kujadili maandalizi ya Tanzania kuelekea Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama Wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP 31).
Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Kemilembe Mutasa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wataalaamu kutoka taasisi za umma, sekta binafsi na wadau wa maendeleo wakati wa kikao cha wataalamu kilichofanyika tarehe 27, Oktoba 2026 Jijini Dar es Salaam kujadili maandalizi ya Tanzania kuelekea Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP 31)
Wataalamu kutoka taasisi za umma, sekta binafsi na wadau wa maendeleo wakifuatilia kikao cha wataalamu kilichofanyika tarehe 27, Oktoba 2026 Jijini Dar es Salaam kujadili maandalizi ya Tanzania kuelekea Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama Wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP 31).
Wataalamu kutoka taasisi za umma, sekta binafsi na wadau wa maendeleo wakifuatilia kikao cha wataalamu kilichofanyika tarehe 27, Oktoba 2026 Jijini Dar es Salaam kujadili maandalizi ya Tanzania kuelekea Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama Wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP 31).
Wataalamu kutoka taasisi za umma, sekta binafsi na wadau wa maendeleo wakifuatilia kikao cha wataalamu kilichofanyika tarehe 27, Oktoba 2026 Jijini Dar es Salaam kujadili maandalizi ya Tanzania kuelekea Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama Wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP 31).
Wataalamu kutoka taasisi za umma, sekta binafsi na wadau wa maendeleo wakifuatilia kikao cha wataalamu kilichofanyika tarehe 27, Oktoba 2026 Jijini Dar es Salaam kujadili maandalizi ya Tanzania kuelekea Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama Wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP 31).
Wataalamu kutoka taasisi za umma, sekta binafsi na wadau wa maendeleo wakifuatilia kikao cha wataalamu kilichofanyika tarehe 27, Oktoba 2026 Jijini Dar es Salaam kujadili maandalizi ya Tanzania kuelekea Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama Wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP 31).

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »