Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Prof. Peter Msoffe Oktoba 13,2026 ameongoza zoezi la ugawaji maziwa kwa wanafunzi wa shule za msingi na zile za mahitaji maalum zilizopo Halmashauri ya jiji la Tanga na ila ya Mkinga mkoani Tanga.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo Prof. Msofe amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi chini ya mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na mabadiliko ya Tabia nchi imetumia fursa ya uwepo wa Wiki ya chakula Duniani mkoani humo kuhamasisha wanafunzi kunywa maziwa, kula mayai na vyakula vingine vya protini.
“Sisi kwa sababu tunajua nyie ni watoto mkijifunza mkaelewa mtawasaidia watoto wenu pindi mtakapokuwa wazazi hapo baadae” Ameongeza Prof. Msofe.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Sebastian Shilangalila amesema kuwa mkoa wa Tanga ni miongoni mwa mikoa nane ambayo mradi huo umekuwa ukihamasisha matumizi ya maziwa kwa ngazi zote za jamii ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga ni miongoni mwa Halmashauri 21 zinazonufaika na mradi huo.
Naye Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Manza Arafa Mohammed ameishukuru Serikali kwa kuwawezesha maziwa na mayai hayo ambapo ameongeza kuwa vyakula hivyo vitaboresha afya zao pindi wakiwa shuleni na kuongeza ufanisi wao pindi wawapo darasani.






EmoticonEmoticon