KLINIKI YA KODI KILOMBERO NI KICHEKO KWA WALIPAKODI

October 30, 2026

   

Kliniki ya Kodi inayofanyika wilayani Kilombero katika mji mdogo wa Ifakara mkoani Morogoro imetajwa kuleta tabasamu kwa Walipakodi wilayani humo kutokana na kutatuliwa papo kwa hapo kwa changamoto za Kodi zilizokuwa zikiwakabili kwa muda mrefu. 

Katibu wa wafanyabiashara wilayani Kilombero Bi. Lilian Mlekia amesema wafanyabiashara wilayani humo walikuwa na shauku ya kutatua changamoto za kodi zilizokuwa zikiwakabili na Kliniki hiyo imekata kiu zao baada ya changamoto zao kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo. 

Amemshukuru Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Yusuph Juma Mwenda kwa kutekeleza ahadi yake aliyoitoa Oktoba 19, 2026 ya kuweka Kliniki ya Kodi kwenye eneo lao ili kuwasikiliza na kueleza kuwa wamesikilizwa, wameelimishwa na kushauriwa.

Kwa upande wake mshauri wa kodi Bw. Christopher Kitaluma amesema Kliniki hiyo imekuwa msaada kwa walipakodi ambao amekuwa akiwapatia huduma kwani wameongezewa uelewa na kutatuliwa changamoto zao hali ambayo itaboresha zaidi biashara zao na kuongeza utii wa kodi kwa hiari na kwa wakati. 

Naye Meneja wa TRA Mkoa wa Morogoro Bi. Husna Nyange amesema muitikio wa wananchi kupata huduma katika Kliniki hiyo ya Kodi umekuwa ni mkubwa na kuwataka wananchi ambao bado hawajahudumiwa wafike katika ofisi za TRA wilaya ya Kilombero zilizopo kwenye mji mdogo wa Ifakara kupatiwa huduma. 

Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »