𝑴𝑨𝑲𝑨𝑴𝑼 𝑾𝑨 𝑹𝑨𝑰𝑺 𝑨𝑾𝑨𝑩𝑨𝑡𝑨 𝑾𝑨𝑲𝑨𝑡𝑫𝑨𝑹𝑨𝑺𝑰 𝑲𝑨𝑻𝑨𝑽𝑰, 𝑨𝑻𝑢𝑨 𝑲𝑰𝑲𝑢𝑴𝑢 π‘ͺ𝑯𝑨 𝑫𝑬𝑺𝑬𝑴𝑩𝑨 𝑲𝑾𝑨 𝑴𝑹𝑨𝑫𝑰 𝑾𝑨 𝑼𝑴𝑬𝑴𝑬 𝑴𝑷𝑨𝑡𝑫𝑨.

October 13, 2026

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi,ameagiza kuharakishwa kwa miradi ya barabara, maji na umeme mkoani Katavi, huku akiwataka wakandarasi wanaosuasua kuongeza kasi ya utekelezaji ili wananchi waanze kunufaika na uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali.

Maagizo hayo ametoa alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Mpanda, akiwa njiani kuelekea Sumbawanga mkoani Rukwa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, ambapo alipata fursa ya kuwasalimia wananchi waliojitokeza kumpokea.

Akizungumzia changamoto ya umeme, Makamu wa Rais ameitaka TANESCO kuhakikisha kufikia Desemba 01 2026, Mpanda inapelekewa Transfoma itakayoongeza megawati 50 zaidi za umeme ili kukidhi mahitaji yanayozidi kuongezeka katika Manispaa ya Mpanda na maeneo mengine ya mkoa huo.

Makamu wa Rais amesisitiza kuhakikisha ahadi ya kukamilisha maboresho hayo inatekelezwa, sambamba na kuweka nguzo za zege.
















Share this

Related Posts

Previous
Next Post »