TRA YAENDELEA KUWASOGEZEA HUDUMA WALIPAKODI, YASISITIZA ULIPAJI KODI KWA WAKATI

September 24, 2026
Kariakoo, 23 Septemba, 2026

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mkoa wa Kikodi Kariakoo, leo imefanya ziara kwa walipakodi mbalimbali kwa lengo la kusikiliza na kufahamu changamoto zinazowakabili katika utekelezaji wa majukumu yao ya kikodi, pamoja na kuzitafutia ufumbuzi kwa wakati.

Aidha, ziara hiyo imelenga kuwashukuru walipakodi kwa ushirikiano wanaoutoa kwa Mamlaka, sambamba na kuwakumbusha kutekeleza wajibu wao wa kulipa kodi kwa wakati, hususani kwa awamu hii ya tatu ya mwezi Septemba 2026.

Katika ziara hiyo, uongozi wa TRA Mkoa wa Kikodi Kariakoo umetembelea Zanzibar Insurance Corporation (ZIC), Nazneen General Handling Co., Diamond Global Terminal pamoja na Tanzania Football Federation (TFF) na kuwapa fursa ya kueleza changamoto na hoja mbalimbali zinazohusiana na masuala ya kodi, huku wakipatiwa ufafanuzi kuhusu namna ya kuzitatua na kuendelea kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »