Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe.Balozi, Dr. Batilda Burian amezindua zoezi la utoaji wa chanjo ya Polio awamu ya pili kwa Watoto walio chini ya umri wa miaka 10, katika Mkoa huo, ambapo uzinduzi huo umefanyika katika Shule ya Msingi Bombo Jijini Tanga, ambapo amesema kuwa njia pekee ya kuepuka Ugonjwa wa Polio ni Watoto kuwahi kupatiwa chanjo
![]() |
Chanjo hiyo imezinduliwa leo septemba 29 na inaendelea hadi Oktoba 2,2026
“Ugonjwa wa polio hauna matibabu,hauna Dawa, lakini unaweza ukawahi kwa kupatan chanjo. Sasa mtoto ambaye anaumri chini ya miaka 10, asipopata hii chanjo Matokeo yake baadae, maana sisi nchi yetu siyo kisiwa, tuna majirani zetu wanaweza wakaja ambae amepata polio huko ikawa rahisi kuambukiza Watoto wetu - Dr. Burian".
.jpg)



EmoticonEmoticon