DCP MISIME AONGOZA KIKAO KAZI CHA MAAFISA HABARI

September 30, 2026


Msemaji wa Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) David Misime leo asubuhi Septemba 30,2026 akiwa kwenye ukumbi wa Shule ya Polisi Tanzania - Moshi kuendelea kuongoza kikao kazi cha kuwajengea uwezo Maafisa Habari kutoka Makao Makao Makuu ya Polisi, Mikoa, Vikosi na Vyuo vya Polisi ikiwa ni siku ya tatu.

Mafunzo hayo ya siku tatu malengo yake ni kuwajengea  uwezo Maafisa Habari wa Polisi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi ili wananchi waendelee kupata elimu ya masuala kiusalama na kujenga ushirikiano endelevu katika kubaini na kuzuia uhalifu na kutatua changamoto zinazowakabili kabla ya kukua na kuwa uhalifu.

Pia, kikao hicho kinalenga kuwajengea uwezo  ili wawe na uwezo zaidi wa kuendelea kuimarisha mahusiano na vyombo vingine vya Habari sambamba na kuweza kutekeleza majukumu yao kulingana na mazingira ya sasa ambayo teknolojia ya mawasiliano inabadilika kila siku.

Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »