REA YANG'ARA SABASABA 2026

July 13, 2026




🏆 *RAIS MWINYI ASHUHUDIA REA IKITWAA TUZO YA MUONESHAJI BORA WA TAASISI ZA SERIKALI*


🤝 *REA YAWASHUKURU WADAU KWA MCHANGO WAO KATIKA MAFANIKIO HAYO*


📍 Dar es Salaam


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameshuhudia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ukitwaa Tuzo ya Muoneshaji Bora wa Taasisi za Serikali (*Government Institutions Exhibitor*) katika kilele cha Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) 2026.


Tuzo hiyo imepokelewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma wa REA, Bi. Martha Chassama, kwa niaba ya Wakala.


REA inawashukuru wadau wote waliotembelea banda lake, kujionea mafanikio na utekelezaji wa miradi ya nishati vijijini, pamoja na kuendelea kuunga mkono jitihada za Wakala za kupeleka nishati ya umeme kwenye vitongoji. 


Mwisho

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »