Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Uledi Mussa, ameipongeza TRA kwa mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa majukumu yake ya ukusanyaji mapato na utoaji huduma kwa walipakodi.
Amesema mafanikio hayo yanapaswa kuwa chachu ya kuongeza bidii zaidi ili kufikia malengo makubwa ya taasisi na Taifa kwa ujumla.
Akizungumza Julai 10, 2026 wakati wa kuhitimisha kikao cha utendaji kazi wa TRA, kwa kipindi cha mwaka 2025/2026 Bw. Mussa ameitaka taasisi hiyo kuendelea kudumisha kasi ya mafanikio yaliyopatikana kwa huku ikiimarisha zaidi uhusiano na Walipakodi.
Amesisitiza kuwa juhudi za pamoja na nidhamu ya kazi ni msingi muhimu wa kuendeleza mafanikio hayo na kueleza kuwa nchi mbalimbali zimekuwa zikijifunza kutoka kwa mifumo na mbinu zinazotumiwa na TRA katika ukusanyaji wa mapato.
Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Yusuph Juma Mwenda, amewataka viongozi wa taasisi hiyo kuongeza juhudi katika kukuza mahusiano mema na walipakodi pamoja na kushughulikia kwa haraka changamoto zinazowakabili.
Amesema uhusiano mzuri kati ya TRA na walipakodi ni nguzo muhimu katika kufanikisha ukusanyaji wa mapato ya serikali.
Aidha Kamishna Mkuu amewahakikishia Walipakodi kote nchini kuwa TRA itaendelea kutenda haki katika kutoa makadirio ya kodi yanayowiana na kipato cha Mlipakodi husika.








EmoticonEmoticon