MBUNGE ADO SHAIBU AKUTANA NA TANZANIA ONE KUTOKA TUNDURU

July 11, 2026


Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini Mh. Ado Shaibu Ado amekutana na kufanya mazungumzo na Ndugu Biriat Yafet Biriat ambaye kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kwa ngazi ya kidato cha sita ndiye kinara wa kufaulu nchi nzima (Tanzania One)

Mh. Ado amesema ameamua kukutana na mwanafunzi huyo aliyehitimu shule ya Ndanda Wilayani Masasi akitokea Wilayani Tunduru kwa sababu ufaulu wake ambao haujawahi kutokea kwa kiwango hicho Wilayani Tunduru umeiletea heshima kubwa wilaya ya Tunduru.



Mbali na kumpongeza Mh. Ado alikubali maombi ya Ndugu Biriat kusaidiwa simu, laptop na fedha za kujikimu na kushughulikia michakato yote hadi pale atapojiunga rasmi na kupata mkopo wa Serikali. Ndugu Ado alimnunulia simu, kumkabidhi fedha taslimu milioni moja na kumpa ahadi ya kumuagizia laptop. Amesema kuwa atatoa ushirikiano kwa mahitaji mengine ya kielimu yatayoibuka.


Kwa upande wake Ndugu Biriat amemshukuru Ndugu Ado kwa msaada wake akiamini hatua hiyo inafungua milango zaidi kwa wadau wengine.

Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »