WANANCHI WAHOJI UHAKIKI MFUMO WA VIPIMO VYA DATA: “TUNACHOLIPIA HAKITOSHI”

June 21, 2026


Na Okuly Julius, OKULY BLOG, DODOMA


Wakazi wa Jiji la Dodoma wameiomba Serikali kupitia Wakala wa Vipimo (WMA) kuingilia kati na kusimamia ipasavyo matumizi sahihi ya vipimo vya vifurushi vya intaneti “bando” pamoja na muda wa maongezi wakidai kupoteza data zao kwa haraka na bila uwazi.

Wananchi hao wametoa wito wa kuwepo kwa uwazi na ukomo sahihi wa muda wa matumizi ya data, wakisema ni haki yao kupata kile wanacholipia.

Baadhi ya wakazi waliozungumza jijini hapa wameeleza kusikitishwa na namna megabytes (MBs) au gigabytes (GBs) wanazonunua zinavyoisha kwa muda mfupi hata pale wanapokuwa hawatumii simu zao kikamilifu, jambo linaloashiria kasoro kwenye usahihi wa vipimo hivyo

Meneja wa Wakala wa vipimo mkoa wa Dodoma Said Ibrahim, anasema wakala umepokea maoni hayo ya wadau na kuongeza kuwa umeshaanza mchakato wa kusimamia uhakiki ikiwemo katika vifurushi vya intaneti (Bando) na muda wa maongezi.




Share this

Related Posts

Previous
Next Post »