RAIS MSTAAFU DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE AKUTANA NA MHESHIMIWA RAIS WILLIAM RUTO WA KENYA JIJINI NAIROBI

April 16, 2026





Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye ni Mwakilishi wa Ngazi ya Juu wa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kwenye Eneo la Pembe ya Afrika na Bahari ya Shamu jana amekutana na kufanya mazungumzo na Rais William Ruto wa Kenya, Nairobi.

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao walipata fursa ya kuzungumzia mchakato wa kutafuta amani nchini Sudani Kusini, hususan kwa kuzingatia nafasi ya Kenya katika mgogoro wa nchini huo.

Moja ya jitihada za kuleta amani nchini Sudani kusini zimefanywa na Serikali ya Kenya kupitia Mpango wa Amani wa Tumaini ambao umelenga kuvijumuisha katika mazungumzo ya amani vikundi vyote vya kijamii na vya kijeshi ambavyo havikutia saini katika Makubaliano ya Amani nchini Sudani Kusini R-ARCSS yaliyosainiwa Mwaka 2018.

Ziara hii ya Rais Mstaafu Dkt. Kikwete ni sehemu ya kutekeleza kujumu lake jipya la kuwa mpatanishi wa amani nchini Sudani Kusini, ambapo tangu kuteuliwa kwake ameweza kukutana na Viongozi mbalimbali wenye ufuasi katika hali ya amani, ulinzi na usalama nchini Sudani kusini wakiwemo Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, Rais Yoweri Museveni wa Uganda na sasa Rais William Ruto wa Kenya.

Aidha, Dkt. Kikwete ameshafanya ziara nchini Sudani Kusini na kukutana na Makundi yote muhimu katika mgogoro huo kwa lengo la kukubaliana mkakati endelevu utakaohakikisha amani inarejea katika nchi hiyo changa kuliko zote barani Afrika




Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye ni Mwakilishi wa Ngazi ya Juu wa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kwenye Eneo la Pembe ya Afrika na Bahari ya Shamu jana amekutana na kufanya mazungumzo na Rais William Ruto wa Kenya, Nairobi. Picha na IKULU, NAIROBI






Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »