RAIS MSTAAFU DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE AHANI MSIBA WA RAIS WA ZAMANI WA ALGERIA JENERALI MSTAAFU LIAMINE ZEROUL

April 01, 2026

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2026 akitia saini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Rais wa zamani wa Algeria, Jenerali Mstaafu Liamine Zeroual,  aliyefariki dunia mnamo Machi 28, 2026 akiwa na umri wa miaka 84 baada ya kuugua kwa muda mrefu. Pamoja naye ni Balozi wa Algeria nchini Mheshimiwa Ghalib Zermane.  Kitabu hicho kimefunguliwa nyumbani kwa Balozi Oysterbay jijini Dar es salaam.

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2026 ametia saini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Rais wa zamani wa Algeria, Jenerali Mstaafu Liamine Zeroual,  aliyefariki dunia mnamo Machi 28, 2026 akiwa na umri wa miaka 84 baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Jenerali Zeroual, aliyependwa na kuheshimikka sana, alichaguliwa kuwa rais mwaka 1995 katika kipindi kigumu cha vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Algeria. Alianzisha mageuzi ya kisiasa, ikiwa ni pamoja na kuratibu uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi.

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2026 akitia saini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Rais wa zamani wa Algeria, Jenerali Mstaafu Liamine Zeroual,  aliyefariki dunia mnamo Machi 28, 2026 akiwa na umri wa miaka 84 baada ya kuugua kwa muda mrefu. Pamoja naye ni Balozi wa Algeria nchini Mheshimiwa Ghalib Zermane.  Kitabu hicho kimefunguliwa nyumbani kwa Balozi Oysterbay jijini Dar es salaam.

Hata hivyo alijiuzulu mapema mwaka 1998 kabla ya kumaliza muhula wake wa miaka mitano ili kutoa nafasi kwa mpito wa kisiasa, na tangu hapo aliishi maisha ya faragha bila kujihusisha sana na siasa.

Hadi leo anakumbukwa kama kiongozi aliyetoa mchango muhimu katika kuiongoza Algeria katika kipindi cha mpito na changamoto kubwa za kisiasa na kiusalama.

Akiongea na Balozi wa Algeria nchini Mheshimiwa Ghalib Zermane, Dkt Kikwete alisema Algeria na Tanzania imekuwa rafiki wa karibu kwa muda mrefu, na kwamba viongozi wake wote waliopita wamefanya kazi kwa karibu na viongozi wa Tanzania kuanzia Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, hususan hususan katika  ukombozi wa bara la Afrika, akiwataja wataja viongozi hao kama Ahmed Ben Bella, Houari Boumédiène, Chadli Bendjedid,  Liamine Zéroual na Abdelaziz Bouteflika

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »