Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, leo Machi 11, 2026 amefanya kikao kazi cha pamoja na taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati zinazoshughulikia masuala ya mafuta. Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Wizara ya Nishati, Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi, Dkt. James Mataragio, Mkurugenzi Mtendaji wa EWURA, Dkt. James Mwainyekule, pamoja na wataalamu kutoka wizarani na taasisi za TPDC na PBPA.
Lengo la kikao hicho ni kuimarisha ufanisi na usimamizi katika utekelezaji wa majukumu ya taasisi hizo, ili kuboresha utendaji na maendeleo ya sekta ya mafuta nchini.








EmoticonEmoticon