Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imekamilisha kwa asilimia 99 mradi wa kufunga transfoma ya ziada ya MVA 15 katika kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Mahumbika, mkoani Lindi, uliogharimu shilingi milioni 702.
Mradi huu umeimarisha kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa umeme katika Mkoa wa Lindi na wilaya za Masasi, Newala na Nanyumbu mkoani Mtwara.
Akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa ufungaji transfoma hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Mhe. Victoria Mwanziva, ameipongeza Serikali
kwa uwekezaji mkubwa katika sekta ya nishati unaoendelea kuimarisha upatikanaji wa umeme mkoani Lindi na maeneo jirani.
"Ufungwaji wa transfoma hii umeboresha upatikanaji wa umeme na kuchochea maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla". Amesema Mhe. Victoria.
Aidha, viongozi wa Serikali wameahidi kuendelea kushirikiana na TANESCO katika kuhakikisha huduma bora zaidi ya
umeme inapatikana kwa wananchi.





EmoticonEmoticon