Na Mwandishi wetu- DAR ES SALAAM
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI ambaye pia ni Mbunge wa
Arumeru Magharibi Mhe. Johannes Lukumay ameipongeza Serikali kuendelea kusaidia kundi la Watu waishio na Maamubikizi Virusi vya
UKIMWI kupitia shughuli mbalimbali za kiuchumi ili kujikwamua kiuchumi.
Mhe. Lukumay ameyasema hayo tarehe 19 Machi 2026 mara baada ya ziara ya kutembelea Baraza la Watu waishio na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI akiwa ameambatana na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI katika ( Konga ya Jiji) iliyofanyika katika Viwanja vya Pugu Mnadani Jijini Dar es Salaam.
![]() |
Amesema kuwa watu waishio na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI ni sawa na watu wengine hivyo yapaswa kuwapa kipaumbele katika fursa mbalimbali za kimaendeleo.
Pia Mwenyekiti huyo amelipongeza kundi hilo kwa namna
wanavyojituma katika kuhakikisha wanajikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini hivyo kuziagiza sekta husika kusaidia katika kuwatafutia masoko kwa ajili ya bidhaa zao.
Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga amesema kuwa Serikali chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wataendelea kuunga mkono jitihada zao kwa kuongeza nguvu zaidi kwa Wanakonga ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Mhe. Nderiananga amempongeza Mkurugenzi wa Jiji, Mkuu wa Wilaya pamoja na Katibu Tawala wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam na timu nzima kwa kuwawezesha Wanakonga katika fursa mbalimbali na kuwataka kuendelea na desturi hiyo ya kuwawezesha kwani mwaka huu wa fedha bado haujamalizika.
Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Elihuruma Mabelya amesema kuwa moja ya eneo waliloliwekea nguvu ni Konga hiyo kwa kuunga mkono shughuli zao za kiuchumi ili kuhakikisha
wanainuka na kufanikiwa katika nyanja mbalimbali za maendeleo.
![]() |












EmoticonEmoticon