WATOA HUDUMA YA LPG PWANI WAKUMBUSHWA USALAMA

February 24, 2026

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Mashariki imewakumbusha wafanyabiashara na wadau wa gesi ya kupikia (LPG) kuzingatia usalama, afya na utunzaji wa mazingira, wakati wa kusafirisha, kuhifadhi na kuuza bidhaa hizo kwa wateja.

Meneja wa EWURA Kanda ya Mashariki, Mhandisi Lorivii Long’idu, akizungumza wakati wa semina ya wadau hao iliyofanyika mkoani Pwani, 24 Februari 2026 aliwasisitiza wafanyabiashara wa jumla wa LPG kuwa na mikataba na wasambazaji wao na wauzaji wa rejareja wa bidhaa hiyo ili kukidhi matakwa ya kisheria na kiusalama.

Mhandisi Long’idu aliwahimiza pia wadau hao kuwaelimisha wasambazji na wauzaji wa rejareja wa LPG kuhusu usalama na umuhimu wa kutumka mizani iliyohakikiwa na Wakala wa Vipimo wakati wa kutoa huduma ili wananchi wapate huduma bora.

Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »