
📌Vitongoji 173 kupelekewa umeme kwa bilioni 28.3
📌Mkandarasi atakiwa kutekeleza mradi kwa kasi
📍Songwe
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Jabiri Makame ameishukuru Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), kwa kutoa kiasi cha shilingi bilioni 28.3 kupeleka umeme kwa wateja 6,135 waliopo kwenye vitongoji 173 mkoani humo.
RC Makame ametoa pongezi hizo leo Februari 2, 2026 mara baada ya kukutana na Wataalam kutoka REA waliofika kumtambulisha mkandarasi wa mradi wa HEP 2B kampuni ya M/s Jaitech Company Ltd atakayetekeleza mradi wa kupeleka umeme vitongojini.
"Namshukuru sana Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutuletea fedha hizi ili kupeleka umeme kwa wananchi wapatao 6,135 wa mkoa huu ili watumie nishati ya umeme," Amesema RC Makame.
Vilevile, amemtaka mkandarasi wa mradi kutekeleza mradi huo kwa kasi na weledi kwa kuwa wananchi wanamatumaini ya kuwashiwa umeme huo mapema ili waendelee na shughuli za kiuchumi na kuwaletea maendeleo.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa REA, Bw. Frank Mugogo ameeleza kuwa REA itaendelea kutekeleza miradi ya nishati ya umeme vijijini kwa ubora na uhakika ili wananchi wapate umeme wa uhakika.


EmoticonEmoticon