BARRICK YAPONGEZWA KWA KUWEKA MIUNDOMBINU YA KITUO CHA MICHEZO BUZWAGI

February 28, 2026

    

Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakiwa katika picha ya pamoja na Rais wa shirikisho hilo Wallace Karia na Meneja wa Ufungaji wa Mgodi wa Barrick Buzwagi, Mhandisi Zonnastraal Mumbi.
Meneja wa Ufungaji wa Mgodi wa Barrick Buzwagi, Mhandisi Zonnastraal Mumbi akitoa maelezo kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia na ujumbe wake walipotembelea kituo cha michezo cha Buzwagi.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia na ujumbe wake wakitembelea maeneo mbalimbali ya kituo cha michezo cha Buzwagi.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia na ujumbe wake wakitembelea maeneo mbalimbali ya kituo cha michezo cha Buzwagi.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia na ujumbe wake wakitembelea maeneo mbalimbali ya kituo cha michezo cha Buzwagi.


**
Mgodi wa Barrick Buzwagi ambao uko katika mchakato wa kufungwa kwa kushirikiana na Serikali umepongezwa kwa kuweka miundombinu ya kituo cha michezo ambacho kitasaidia kukuza mchezo wa soka na michezo mingineyo nchini.

Pongezi hizo zimetolewa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia, alipoongoza wajumbe wa Mkutano Mkuu wa taifa wa shirikisho hilo kutembelea eneo hilo ambapo amesema miundombinu iliyopo inaridhisha.

Amesema miundombinu hiyo kuanzia nyumba za malazi kwa wanamichezo, viwanja vya michezo, usalama, pamoja na mazingira yake kwa ujumla ipo katika hali nzuri na inakidhi mahitaji ya kuanzishwa kwa kituo hicho.

“Natoa shukrani kwa kampuni ya Barrick na Serikali kwa kukubali ombi la kuanzishwa kituo cha michezo katika eneo la mgodi uliofungwa, tunafurahi kuona kituo kiko katika hali nzuri na kina viwango vikubwa kwa ajili ya kuhudumia wanamichezo, hii ni fursa muhimu kwa maendeleo ya michezo yetu”, amesema.

Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Taifa ya TFF, Azan Mufti, amesema kutengwa kwa eneo hilo kwa ajili ya wanamichezo kunadhihirisha ushirikiano mzuri uliopo kati ya sekta binafsi na wadau wa sekta ya michezo katika kufanikisha ajenda ya Serikali ya kukuza vipaji na kuendeleza michezo nchini.

Naye Meneja wa Ufungaji wa Mgodi wa Barrick Buzwagi, Mhandisi Zonnastraal Mumbi, amesema kutengwa kwa eneo la kujengwa kituo cha michezo katika eneo hilo la mgodi uliofungwa kumezingatia dhamira ya kampuni ya kusaidia jamii sambamba na kuunga mkono jitihada za serikali za kukuza vipaji na kuchochea maendeleo ya michezo nchini.

Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »