Na Oscar Assenga, TANGA
BENKI ya Maendeleo ya TIB imesema kwamba lengo lao ni kuendelea kuchochea ukuaji wa maendeleo nchini kupitia uwekezaji kwa kuangalia miradi yote mikubwa kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo Tanzania Deogratius Kwiyukwa wakati wa maonesho ya tano ya wiki ya huduma za Fedha ambapo alisema katika uwekezaji kwa kuangalia miradi yote mikubwa iwe ya Serikali na Binafsi kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali.
Alisema kwamba katika upande wa maji wanashirikiana na Water Fund kuhakikisha wananchi wanapata maji kwa upana zaid kwa maana ya kutengeneza tija kwao ili kuweza kujikwamua kiuchumi.
Aidha alisema katika kuhakikisha uwekezaji huo unakuwa na tija kubwa wanashirikiana pia na REA kuhakikisha wanapata umeme hasa vijijini na wale wawezekaji katika nishati ya umeme wanapata fund kwa wakati.
Aidha alisema kwamba baada ya hapo wanaingiza wao kwenye gridi ya Taifa ni Benki ambayo inaanfalia miradi mipana ya Serikali na watu binafasi kuhakikisha zile changamoto ambazo wajasiriamali wanazo wanazifanyia kazi.
Alisema pia benki yao ina tofauti na benki nyengine kwa maana wanachukua muda mrefu katika miradi mpaka miaka 15 pamoja na muda mfupi kutokana na aina ya mradi na wapo kimkakati hatua inayopelekea mchango mkubwa sana kwa maendeleo ya nchi ya Tanzania
“Sisi Benki ya TIB katika kuchochea maendeleo Tanzania na tupo kwenye sekta zote nchini kama wadau wakubwa kuhakikisha nchi hasa katika upande wa viwanda ambavyo pia ndani yake vinachochea ajira wanashirikiana na taasisi mbalimbali binafsi na serikali kuhakikisha wanatengeneza ajira”Alisema
Alisema kwamba na wanapochochea uwepo wa viwanda hata uagizaji wa bidhaa kutoke nje ya nchi unapungua maana yake wataweza kuokoa fedha za kigeni na kuweza kutumia fedha ndani kuliko kuagiza kutoke nje ya nchi.
Katika hatua nyengine alaisema kwa upande wa Kilimo benki hiyo wana dirisha ambalo wanatoa mikopo kuanzia asilimia 3 mpaka 4 kwa wawekezaji ambao wanawezeka kwenye mnyororo mzima wa sekta ya Kilimo.
Alisema kwamba huo ni mchango wao mkubwa kuhakikisha wawekezaji wanaokwenda kuomba mikopo wanapata kwa wakati ili kuenda kuzalisha na kutengeneza ajira mbalimbali kwa Taifa.
Hata hivyo alisema kwamba dhamira yako pia ni kuhakikisha wanawaibua wajasiriamali wadogo wadogo ili waweze kukopesheka na mabenki mengine na kuondokana na changamoto ambazo wanakabiliana nazo ikiwemo za mitaji.
Alisema katika kuhakikisha suala hilo linakuwa na tija wanawajengea uwezo wajasiriamali wanaoanza kuchipukia kuweza kuingia sokoni na kuweza kutafuta mitaji katika maeneo mengine
Alisema kwamba vigezo vya upatikanaji wa mikopo ni kama ilivyo kwa taasisi nyengine za kifedha wanaangalia wazo la biashara, kuangalia mradi wake wana kitengo ambacho kinawashauri wafanye ni kwa kupatiwa muongozo ili aweze kukubalika na maneki mengine
Mwisho…
EmoticonEmoticon