EWURA YAITIKISA SHIMMUTA, YAILAZA NEMC

December 01, 2025

Pichani: Washambuliaji wa Timu ya EWURA (wenye jezi za bluu) wakishambulia timu pinzani wakati wa mchezo huo leo.

MOROGORO.

 Timu ya Mpira wa Wavu kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) imeendelea kung’ara katika mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMMUTA) baada ya kuichakaza timu ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa seti mbili mfululizo.

Katika mchezo huo uliochezwa leo mkoani Morogoro, EWURA ilipata pointi 25 katika seti zote mbili, huku NEMC ikijitahidi lakini ikibaki na pointi 23 kwenye seti ya kwanza na 17 katika seti ya pili.

Mchezo huo uliovuta hisia za mashabiki ulitawaliwa na kasi, nidhamu na uchezaji wa kimkakati kutoka kwa EWURA, ambao washambuliaji wao walionekana kuwa imara zaidi dhidi ya ngome ya NEMC.

Pichani: Washambuliaji wa Timu ya EWURA (wenye jezi za bluu) wakishambulia timu pinzani wakati wa mchezo huo leo.

Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »