*📌Ni kwenye kutoa elimu ya masuala ya Nishati Safi ya Kupikia
*📌Wananchi wamejitokeza kwa wingi kujipatia majiko ya bei ya ruzuku ya shilingi 17,500/=*
📍Tanga
Ushiriki wa Wizara ya Nishati na taasisi zake (Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) katika Maonesho ya Wiki ya Chakula duniani yanayoendelea jijini Tanga umevutia wananchi wengi kutembelea banda la Wizara ili kupata elimu ya nishati safi ya kupikia sambamba na taarifa mbalimbali kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme, Gesi Asilia na Mafuta.
Miongoni mwa waliotembelea maonesho hayo ni pamoja na Mkurugenzi wa Nishati safi ya Kupikia kutoka Wizara ya Nishati, Bw. Nolasco Mlay, ambapo ameeleza kufurahishwa kwake na namna wananchi wananvyofurika katika banda la Wizara na Taasisi zake kupata huduma mbalimbali.
"Nimevutiwa na muitikio mkubwa wa wananchi wanaofika kuchukua majiko ya gesi kwa bei ya ruzuku ya shilingi 17,500 yanayotolewa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja na kupewa elimu. Hakika sisi tunavutiwa na mwamko huu katika mkoa wa Tanga hasa katika kutekeleza Ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia." Amesema Bw. Mlay
Mlay amewaasa wananchi na watanzania wote kutumia nishati hiyo kwa kuwa ni safi na salama kwa afya ya watumiaji na mazingira.
Ameongeza kuwa, Serikali inaendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi na salama kwa makundi mbalimbali ya wananchi ikiwemo taasisi zinazolisha watu kuanzia 100 ili kufikia lengo la asilimia 80 ya watanzania kutumia nishati safi ya kupikia ifikapo 2034.
#NishatiTupokazin
EmoticonEmoticon