Na Paskal Mbunga,TANGA
Rais Samia anatarajiwa kufanya ziara ya siku tatu mkoani Tanga itakayoanza Septemba 28, 2025.
Ziara hiyo ambayo ni mwendelezo wa ziara zake za kampeni za kampeni za kujinadi nafasi ya Urais kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi habari katika Makao Makuu ya CCM (M)-Tanga, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa, Ustadh Rajabu Abdrahamani, alisema ujio wa Rais Samia kwa mara nyingine tena mwaka huu, wananchi wategemee maendeleo zaidi kwani baadhi ya miradi ya maendeleo iliyokuwa inasuasua sasa imepata msukumo mpya na hivyo aidha kukamilika au kufikia hatua nzuri ya kukamilika.
Aliitaja baadhi ya miradi ya maendeleo ambayo imepata msukumo kutokana na ziara ya Rais ni pamoja na mradi mkubwa wa barabara ya Tanga-Pangani-Bagamoyo. Barabara nyingine ni Soni-Bumbuli-Dindira-Korogwe kupi tia Kwameta.omg
Meenyekiti huyo wa CCM wa Mkoa wa Tanga alibainisha kuwa iwapo wananchi watamchagua kwa kumpa kura nyingi katika uchaguzi wa mwezi Oktoba 29, Watanzania wategemee maendeleo zaidi kwaewa Mkoa wa Tanga.
Ziara hii ya Rais Samia mkoani hapa imeuheshimisha Mkoa wa Tanga kwani umetembelewa na wagombea wa nafasi za Urais na Makamu wa Rais katika uchaguzi wa mwaka huu kwa vipindi tofauti.
Wiki mbili zilizopita, Mkoa wa Tanga ulitembelewa na Balozi Emanuel Nchimbi, mgombea nafasi ya Makamu wa Rais kupitia CCM, akiwa katika kampeni yake Mkoani hapa alifanya kampeni katika wilaya zote isipokuwa wilaya za Tanga na Pangani.
Mwenyekiti Rajabu alifafanua kwamba baada ya kuwasili jijini Tanga jioni ya Septemba 28, atapumzika ambapo siku iliyofuata ataelekea wilaya ya Pangani ambako atakuwa na mkutano wa hadhara mjini humo na baadaye kurejea Tanga ambapo atahutubia mkutano mkubwa wa hadhara na kisha kuhitimisha ziara yake ya siku tatu akipitia wilaya za Muheza na Korogwe.
(Mwisho)
EmoticonEmoticon