Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Famamu Muhimbili (MOI) Dkt Marina Njelekela,akizungumza wakati akifungua kikao cha pili cha Baraza la Wafanyakazi wa Taasisi hiyo kilichofanyika leo Septemba 8,2025 jijini Dodoma.
Na Mwandishi wetu, Dodoma
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan imewezesha Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Famamu Muhimbili (MOI) kutoa huduma bora za ubingwa bobezi kwa ununuzi wa vifaa vya kisasa ikiwemo CT SCAN mbili, MRI, mbili Angio Suite, Ultrasound na X-Ray za kisasa.
Hayo yemesemwa leo Septemba 8, 2025 jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini MOI Dkt Marina Njelekela wakati akifungua kikao cha pili cha Baraza la Wafanyakazi wa Taasisi hiyo.
"Hili ni jambo la kujivunia na kuishukuru Serikali yetu ya Awamu ya Sita, niwaombe tuendelee kuvitunza na kuvithamini vifaa hivi ili viendelee kuwanufaisha wananchi", alisisitiza Dkt Njelekela
Akieleza zaidi Dkt Njelekela amesema Menejimenti ya Taasisi hiyo iendelee kuwakumbusha watumishi kufuata misingi ya maadili katika kuhudumia wananchi kwa kufanya kazi kwa bidii kama wanavyofanya sasa.
"Ninafurahi kwamba MOI tumeendelea kufanya kazi kwa bidii bila kuchoka, naomba niwapongeze kwa hilo. Naomba niwahakikishie kwamba Bodi yenu iko kazini na itaendelea kushirikiana uongozi wa Taasisi ya MOI katika kuboresha huduma za kibobezi za Matibabu ya Mifupa, Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu", alisisitiza Dkt Njelekela
Akifafanua, Dkt Njelekela amesema "kikao hicho kijikite kufanya majadiliano ya kina na busara kwa kuweka mikakati thabiti na utekelezaji wake na sisi kama bodi ya wadhamini tutaendelea kushirikiana nanyi kwa kila jambo. Kwa mamlaka niliyopewa napenda kufungua rasmi kikao cha pili cha Baraza la Sita la Wafanyakazi wa Taasisi ya MOI," alisisitiza Dkt Njelekela
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Mpoki Ulisubisya amesema "Tunayo miradi ya kimkakati ambayo inaendelea katika Taasisi yetu ya MOI ikiwemo; Mradi wa New OPD ambao umekamilika kwa asilimia 25% na Mradi wa X-Tumaini ambao na wenyewe umekamilika kwa asilimia 95% ",
Mbali na hayo, Dkt Ulisubisya amesema wamefanya ukarabati wa jengo la MOI Phase III (kupaka rangi) na maboresho ya wodi zetu za private (level 6) yanaendelea.
"Nafahamu kwamba tunayo kiu ya kuangalia namna ya kuboresha maslahi ya watumishi wetu kama tulivyowahi kuelezana hapo awali, tunahitaji kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza mapato ambayo yateendena na mahitaji yetu pamoja na maboresho ya huduma na kulipa wazabuni", alisisitiza Dkt Ulisubisya
Pia, aliwataka wajumbe wa Kikao hicho kuwa vielelezo vyema kwa wale tunaowaongoza kwa kiwa kiunganishi na kuwafanya watumishi waipende kazi yao.
"Naomba kuwashukuru kwa kazi nzuri mnayofanya na kujenga jina na taswira nzuri ya Taasisi yetu. Hivi karibuni iliibuka mijadala kwenye mitandao ya kijamii ya kupongeza baadhi ya watumishi wetu hii ni ishara kwamba wananchi wanaridhika na huduma zetu", alisisitiza Dkt Ulisubsya
Katika kuimarisha huduma zake MOI inatumia majukwaa ya mitandao kijamii ikiwemo makundi sogozi ya whatsapp kupokea maoni kutoka kwa wananchi na kuwasiliana nao ili kuendelea kuimarisha huduma.









EmoticonEmoticon