MAENDELEO MAKUBWA YANAKUJA MOROGORO - WASIRA

September 12, 2025

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, akizungumza katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika viwanja vya Lupiro jimboni ambapo alimuombea kura Mgombea wa Ubunge jimbo la Ulanga Ndg. Salim Alaudin Hasham pamoja na Madiwani wa CCM na Mgombea wa Kiti Cha Urais Kupitia CCM Dkt Samia Suluhu Hassan.

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, akizungumza katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika viwanja vya Lupiro jimboni ambapo alimuombea kura Mgombea wa Ubunge jimbo la Ulanga Ndg. Salim Alaudin Hasham pamoja na Madiwani wa CCM na Mgombea wa Kiti Cha Urais Kupitia CCM Dkt Samia Suluhu Hassan.




MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, akimuombea kura Mgombea wa Ubunge jimbo la Ulanga Ndg. Salim Alaudin Hasham katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika viwanja vya Lupiro jimboni hapo.




*Wasira asema Ilani imeipa kipaumbele cha kujengwa barabara kero kwa wananchi

*Sasa kuunganishwa kwa lami na mkoa jirani wa Ruvuma ili kufungua uchumi wake

*Amwombea kura mgombea urais kupitia CCM Dk. Samia Suluhu Hassan

Na Mwandishi Wetu, Malinyi

CHAMA Cha Mapinduzi kimeeleza namna kitakavyoifungua Morogoro kwa ujenzi wa barabara ya lami itayounganisha mkoa huo na mkoa jirani wa Ruvuma.

CCM imewahakikishia wananchi kuwa katika Ilani yake ya Uchaguzi ya 2025-2030 itawafikia zaidi wakulima kwa kuendelea kutoa ruzuku ya mbolea na mbegu.

Wasira alieleza hayo kwa nyakati tofauti akizungumza na wana CM na wananchi katika vikao vya ndani vya Chama na mikutano ya kampeni katika majinbo ya Malinyi na Ulanga, wilayani Malinyi, Mkoa wa Morogoro, jana.

"Tutafanya nini miaka mitano ijayo?, kwanza tutaendelea kuimarisha elimu maana elimu ndio msingi wa maendeleo na tunakusudia kujenga barabara ya kutoka Ifakara kuja Lupilo mpaka Malinyi, ipo katika Ilani na hiyo ni barabara moja tu.

"Tunajenga barabara inayounganisha Morogoro na Songea (mkoa wa Ruvuma) nayo itapita hapa hapa (Malinyi), wala siyo ndoto, makandarasi katika maeneo mengine wapo, tunataka kufungua eneo hili la Morogoro kwa sababu kwa muda mrefu limekuwa na miundombinu yenye matatizo," alisema.

Alisema kuondoa matatizo ni jujuju na kazi ya CCM, hata hivyo haiwezi alisema changamoto haziwezi kumalizwa kwa wakati mmoja.

Alisema katika ilani hiyo CCM imeielekeza serikali kusudi la kujenga madaraja mawili yanayosumbua katika barabara ya Ifakara-luoiro-Malinyi na Lupiro-Mahenge.

"Shabaha yetu ni kufungua eneo hili, eneo hili ni muhimu sana kwa uchumi, ndiyo, ninyi mnalima sana mpunga na lazima tuweke barabara mpunga ufike sokoni ili kazi yenu iwalipe kwa sababu mkifika sokoni bei ya mazao yenu itakuwa nzuri na ikiwa nzuri umaskini utapungua.

"Hizo ndizo ahadi za CCM, ahadi za ukweli na zinazotekelezeka, lakini bado tutajenga vituo sita vya afya katika eneo hili katika muda wa miaka mitano ijayo," alieleza.

Mbali na ahadi hiyo, alisema CCM itaielekeza serikali kuendelea kuimarisha miundombinu muhimu kwa ajili ya kuleta mageuzi ya kiuchumi kwa mkoa huo na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wa sekta ya kilimo alisema CCM kupitia serikali itakayoiunda baada ya kupewa ridhaa kwa kuchaguliwa Oktoba 29, mwaka huu, inakusudia kujenga mabwawa ya umwagiliaji maji kwa wakulima wa mpunga.

"Pembejeo kubwa ya mpunga ni maji, ukiwa na maji unalima hata mara mbili na unavuna, tunataka kujenga mabwawa na hapa kuna maji yanasumbua yanafanya mafuriko, sasa lazima tutafute namna kuyakimbiza nyumbaji yatuletee chakula, tutajenga mabwawa.

'Tunajua mnalima mpunga kwa matatizo, mnalima kwa mkono sasa tunataka kuanzisha vituo vya matrekta ili mkulima awe anakodi anakwenba kulima, kama hana uwezo atakopa nusu alipe akishavuna akiuza analipa," alisema.

Alisema CCM kupitia serikali yake itaendelea kutoa ruzuku ya mbegu na mbolea kwa wakulima, kwa kuwa Chama kina kazi ya kuondoa umaskini katika nchi ambao hata hivyo hauwezi kuondoka bila kuwekeza katika sekta inayowafaa wakulima.

Pia, Wasira alisema Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2030 imeaijisha dhakira yake ya kuanzisha viwanda vinavyoambatana na mazao yanayopatikana mkoani Morogo hususan eneo la Malinyi.

"Hapa tunataka kuweka viwanda vitakavyokoboa mpunga vinavyochambua kati ya mpunga na mchele, tufungashe na kwa kutumia miundombinu ya barabara mazao ya Malinyi yanaweza kufika sokoni popote katika Afrika Mashariki," alisisitiza

Kupitia viwanda hivyo alisema vitatoa ajira kwa vijana wasio na ajira ambapo pia uwepo wa matrekta yatawapa vijana hamasa ya kulima kwa sababu wengi wao wanaogopa jembe la mkono.

Mgombea ubungs Jimbo la Ulqnga, Salim Almasi aliwahakikishia sananchi wa jimbo hilo iwapo watampa ridhaa ya kwenda tena bungeni atasukuma na kusimamia vema ajenda ya maendeleo kwa jimbo hilo.

Kwa upande wake mgombea ubunge wa jimbo la Malinyi Dk. Mecktridis Mdaku, alisema kutokana na imani kubwa aliyopewa na Chama na wna CCM wa jimo hilo hatalala kuhakikisha yaliyoahidiwa katika ilani ili kuwaletea maendeleo wananchi.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »