Imbeju yatoa mikopo ya shilingi milioni 555.6 kwa wajasiriamali Kigoma

September 27, 2025



Programu ya Imbeju inayotekelezwa na Taasisi ya CRDB Bank Foundation imetoa zaidi ya shilingi milioni 555.6 kwa vikundi 58 vya wajasiliamali mkoani Kigoma.

Mikopo hiyo itokanayo na asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri imekabidhiwa na Mkuu wa Wilaya Kigoma, Dkt. Rashid Chuachua akiwa sambamba na Meneja Mwandamizi wa Uwezeshaji wa CRDB Bank Foundation, Baraka Kilayo.

Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji ni kati ya mamlaka 10 za serikali za mitaa zilizochaguliwa na serikali kutoa mikopo jumuishi kwa wajasiriamali kwa kuzishirikisha taasisi za fedha.

Baada ya kutolewa kwa hundi hiyo, kunaifanya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kufikisha kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 600 ilizozitoa kwa vikundi vya wanawake, vijana na makundi maalumu ambao ndio wanufaika wakuu wa mikopo hiyo.

Mkuu wa wilaya Kigoma Dkt. Rashid Chuachua akizungumza na vikundi vya Wanawake, vijana na walemavu waliopokea mikopo inayotolewa na Halmashauri ya manispaa ya Kigoma Ujiji kupitia Benki ya CRDB chini ya Program yake bunifu ya imbeju.
Meneja Mwandamizi wa Uwezeshaji wa CRDB Bank Foundation, Baraka Kilayo akizungumza wakati wa hafla ya benki hiyo kukabidhi mikopo kwa wajasiliamali wa manispaa ya Kigoma kutoka mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri hiyo kupitia Benki ya CRDB.
Mkuu wa wilaya Kigoma Sk.Rashid Chuachua (mwenye suti ya Bluu) akikabidhi hundi kwa vikundi vya Wanawake, vijana na walemavu mikopo inayotolewa na Halmashauri ya manispaa ya Kigoma Ujiji kupitia Benki ya CRDB kupitia Program ya imbeju.

Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 735 997 777 www.kajunason.blogspot.com "Everything is Possible Through Peace & Stability'' >>> DO YOUR PART TO PREVENT COVID-19: • Wash your hands frequently • Avoid touching face • Cover coughs and sneezes • Disinfect surfaces regularly • Limit handshaking • Consider postponing travel plans • Avoid large gatherings

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »