MGOMBEA mwenza wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel John Nchimbi amewahutubia Wananchi wa Mjini Njombe,waliohudhuria mkutano wake wa hadhara wa kampeni huku akiwaomba ifikapo Oktoba 29 mwaka huu wakipigie kura Chama hicho ili kishinde kwa kishindo.
Dk.Nchimbi ameyasema hayo leo Septemba 23,2025 alipokuwa katika uwanja wa Stendi ya zamani, mkoani Njombe ambapo ametumia nafasi hiyo kutoa ahadi kwa wananchi wa Njombe endapo wataichaguwa CCM basi Ilani ya chama chake imepanga kufanya mipango mingi ya maendeleo mkoani humo.
Maendeleo hayo ni katika maeneo mbalimbali yakiwemo katika sekta ya afya, elimu, kilimo, maji pamoja na kuinua biashara mbalimbali.
Pia Dkt.Nchimbi alitumia nafasi hiyo ya kumnadi Mgombea Ubunge wa jimbo la Jombe Mjini,Ndugu Deodatus Philip Mwanyika pamoja na Madiwani wa jimbo hilo.
Dkt Nchimbi anaendelea na mikutano yake ya kampeni nchi nzima, kusaka kura za ushindi wa kishindo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),ambapo mpaka sasa amefika mikoa 13.
![]() |
EmoticonEmoticon