DKT.NCHIMBI AMALIZA ZIARA RUKWA,AELEKEA KATAVI KUENDELEA NA KAMPENI

September 09, 2025


#HABARI : MGOMBEA Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, amemaliza ziara yake ya kampeni mkoani Rukwa na sasa anaelekea mkoani Katavi kuendelea na harakati za kuomba kura za wananchi.


Akiwa mkoani Katavi, Dk. Nchimbi ataanza kwa kufanya mkutano mdogo katika eneo la Maji Moto kabla ya kuelekea Mpanda Mjini ambako atahitimisha ziara hiyo kwa mkutano mkubwa wa kampeni.



Katika mikutano yake, Dk. Nchimbi ameendelea kunadi Sera na Ilani ya CCM, akisisitiza dhamira ya chama hicho kuendeleza maendeleo yaliyopatikana katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu, kilimo na miundombinu.


Amesema CCM inayoomba ridhaa ya wananchi kwa kipindi cha miaka mitano ijayo, imejipanga kuhakikisha huduma za kijamii zinaimarishwa na fursa za kiuchumi zinaongezeka kwa manufaa ya Watanzania wote.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »