DKT.NCHIMBI AAGANA NA SIMIYU KWA KISHINDO AKIELEKEA SHINYANGA KUSAKA KURA ZA USHINDI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

September 03, 2025

Wananchi  wa Mji Mdogo wa  Lalago,Maswa Mashariki wilayani Maswa wakimsikiliza  Mgombea Mwenza wa Urais wa   Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi  wakati akiwahutubia kwenye mkutano mdogo wa hadhara leo Jumatano Septemba 3,2025,wakati akimalizia mkutano wake wa mwisho wa Kampeni mkoani Simiyu.

Katika mkutano huo wa kampeni,Balozi Dk.Emmanuel Nchimbi aliwanadi Wabunge wa Mkoa huo akiwemo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Maswa Mashariki,Dkt.George Vernance Lugomela  na Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi,Mashimba Mashauri Ndaki pamoja na madiwani .

Pamoja na mambo mengine Balozi Dkt.Emmeanuel Nchimbi amekuwa akiinadi Ilani ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030,ambayo kimsingi imelenga kwenda kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa Maendeleo katika miaka mitano ijayo huku akitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM Rais Dk.Samia Suluhu,Mgombea mwenza wa Urais,wabunge na madiwani wa Chama hicho.



Share this

Related Posts

Previous
Next Post »