Na Mwandishi Wetu, TANGA
Mamlaka ya Mapato Nchini TRA Mkoa wa Tanga,imewapiga msasa kwakuwapatia mafunzo juu ya Sheria za kodi na mabadiliko yake,
mafunzo hayo yamefanyika katika Halmashauri zote 11 za Mkoa wa Tanga na kuhitimishwa jana kwa Wafanyabiashara wa Jiji la Tanga.
katika mafunzo hayo, Wafanyabiashara waliiomba Serikali Kupitia Mamlaka ya mapato Tanzania TRA kuhakikisha inatengeneza Mfumo mmoja, ambao utasaidia kwa kila mtanzania anayefanyabiashara kulipa kodi kwa kiwango cha uwezo wa biashara yake.
katibu Jumuiya ya Wafanyabiashara Mkoa wa Tanga, Ismail Masoud, alisema kuwa utoaji wa Elimu mara kwa mara itasaidia Wafanyabiashara kujua umuhimu wa kulipa kodi na sheria zake.
"Utoaji wa Elimu hii itasaidia kutengenza walipa kodi wapya,kwani tusipokuwa na mpango maalumu wa kutengeneza walipa kodi wapya katika nchi yetu kutakuwa walipo kodi wachache,hii ni hatari sana kwa uchumi wa nchi yetu" Alisisitiza Masoud
Kwaupande wake, Daniel Ramadhani ambaye ni Kaimu meneja wa mkoa wa Tanga alisema lengo la Mafunzo hayo kwa wafanyabiashara ni kuwawezesha kujua sheria ya fedha kutokana mabadiliko ya sheria kwaajili ya maborehsoya kodi yanayotokea kila baada ya bunge la bajet ambapo Mamlaka ya mapato Tanzania TRA imepanga kuwafikia makundi yote ambayo inatakiwa kulipa kodi.
Aliongeza kusema kuwa sheria iliuofanyiwa marekebisho ni pamoja na sheria ya ongezeko la kodi ya thamani ambayo kutakuwa zuio la kodi ya thamani ni mauzo ya biadhaa kwa maana ya asilimia tatu ya mauzo ya bidhaa na mauzo ya ya huduma kwa mfano banki na mitandao mengine.
Kwa upande Chama Siliwa Afisa Masidizi wa elimu na mawasiliano wa Mamlaka ya mapato Tanzania TRA kutoka makao makuu alisema wametoa elimu kwa mlipa kodi kutokana mabadiliko ya sheria mpya ya ulipaji wa kodi hivyo tumeamua kuwapa elimu hiyo wazijue wanapoendelea kulipa kodi changamoto kuwa ya watu kutokulipa kodi ni pamoja na uelewa mdogo wa sheria.
MWISHO
EmoticonEmoticon