🗓️ *27 Agosti,2025.*
📍 *Mbinga-Ruvuma* 🇹🇿🌍.
🟩🟩 *MHE.JUDITH KAPINGA ACHUKUA FOMU YA UBUNGE*
📌 *Mbinga Vijijini yaitika Judith Kapinga akichukua fomu ya Ubunge*
📌 *Judith Kapinga awaahidi Wananchi Amani,Upendo na Mshikamano*
📌 *Judith Kapinga aishukuru CCM,Wanachama wa CCM na Viongozi wa CCM*
🟢🟢Naibu Waziri wa Nishati ambaye ni Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbinga Vijijini, *Mhe.Judith Kapinga* mapema tarehe *26 Agosti,2025* amefika Ofisi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kuchukua fomu ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Mbinga Vijijini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi{CCM}✍️.
🟢🟢 *Mhe.Judith Kapinga* amewashukuru Wananchi,Wanachama wa Chama cha Mapinduzi,Wapenzi wa Chama cha Mapinduzi,Bodaboda,Bajaji,Machinga na Mama Ntilie,kwa upendo wao wa Ushirikiano waliouonyesha kwake katika hatua hiyo ya Uchukuaji wa fomu.Aidha, *Mhe.Judith Kapinga* mara baada ya kuchukua fomu akizungumza na Wananchi wa Kata ya Kigonsera ameishukuru CCM,Wanachama wa CCM na Viongozi wa CCM kwa kumuamini na kumteua kupeperusha bendera ya CCM kugombea Ubunge Jimbo la Mbinga Vijijini."Nitaendelea kuimarisha Amani,Upendo na Mshikamano"amesema *Kapinga* ✍️.
*Imetolewa na Ofisi ya Mgombea Ubunge Jimbo la Mbinga Vijijini,tarehe 27.08.2025.*
EmoticonEmoticon