TAMISEMI YAAHIDI KUSHIRIKIANA NA TEMDO KUTUMIA BIDHAA ZA NDANI

October 19, 2025

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bw Adolf Ndunguru,akipata maelezo  wakati akikagua  bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) katika Makao Makuu ya taasisi hiyo leo  Oktoba 19, 2025,  jijini Arusha.

Na.Mwandishi Wetu

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bw Adolf Ndunguru amesema TAMISEMI itaendelea kushirikiana na Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) kwa kuzihamasisha Halmashauri zote nchini kuanza kutumia bidhaa na vifaa tiba vinavyozalishwa na Shirika hilo katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, hususan kwenye sekta za afya, elimu na kilimo.

Bw. Ndunguru ameyasema hayo leo  Oktoba 19, 2025, alipotembelea makao makuu ya TEMDO jijini Arusha, ambako alipata fursa ya kujionea namna bidhaa mbalimbali zinavyozalishwa na kujadili jinsi taasisi zilizo chini ya TAMISEMI zinavyoweza kushirikiana na TEMDO katika miradi ya maendeleo na kimkakati.

Amesema Serikali, kupitia dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, inaendelea kuimarisha sekta ya afya kwa kuhakikisha upatikanaji wa vifaa tiba bora, imara na vyenye gharama nafuu ili wananchi wapate huduma bora za afya katika vituo vyao.

Aidha, Bw. Ndunguru ameisisitiza TEMDO kuendeleza ubunifu katika bidhaa zake ili ziweze kushindana katika soko na kutumika zaidi na hospitali pamoja na vituo vya afya nchini.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah, ameihakikishia TAMISEMI kuwa TEMDO ina uwezo mkubwa wa kutengeneza vifaa tiba kwa viwango vya kimataifa vilivyothibitishwa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) pamoja na Bohari ya Dawa (MSD), na kwamba taasisi hiyo iko tayari kutoa huduma kwa halmashauri zote nchini.

Naye Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TEMDO, Profesa Lazaro Busagala, amesema kuwa taasisi hiyo inazalisha zaidi ya bidhaa 16 zikiwemo vifaa tiba vya hospitali kama majokofu ya kuhifadhia maiti, vichomea taka hatarishi, na vitanda vya aina mbalimbali.

Aidha amesisitiza kuwa bidhaa hizo zinapaswa kufika hadi Zanzibar ili kuongeza pato la taifa, kukuza uchumi na kupunguza uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa TEMDO, Profesa Frederick Kahimba, amebainisha kuwa tangu mwaka 2022 hadi sasa taasisi hiyo imetengeneza zaidi ya vifaa tiba 1,000 vyenye thamani ya shilingi 2,335,133,622/= na wateja wa TEMDO kuwa ni pamoja na MSD, Hospitali ya Bugando-ZRH, Uhuru Hospital, Hospitali za Kanda za Wizara ya Ulinzi, JKT, Jeshi la Polisi, Hospitali ya Wilaya ya Maswa na Hospitali ya Jiji la Arusha (CSR).

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bw Adolf Ndunguru,akizungumza wakati wa ziara ya kukagua bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) katika Makao Makuu ya taasisi hiyo leo  Oktoba 19, 2025,  jijini Arusha.

 Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah,akizungumza wakati wa ziara ya kukagua bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) katika Makao Makuu ya taasisi hiyo leo  Oktoba 19, 2025,  jijini Arusha.

Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TEMDO, Profesa Lazaro Busagala,akielezea  bidhaa zinazozalishwa katika Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO)  iliyopo   jijini Arusha.

Mkurugenzi Mkuu wa TEMDO, Profesa Frederick Kahimba,akitoa taarifa za  bidhaa zinazozalishwa katika Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO)  iliyopo   jijini Arusha.

Wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bw Adolf Ndunguru,(hayupo pichani) akizungumza wakati wa ziara ya kukagua bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) katika Makao Makuu ya taasisi hiyo leo  Oktoba 19, 2025,  jijini Arusha.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bw Adolf Ndunguru,akikagua  bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) katika Makao Makuu ya taasisi hiyo leo  Oktoba 19, 2025,  jijini Arusha.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bw Adolf Ndunguru,akipata maelezo wakati akikagua  bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) katika Makao Makuu ya taasisi hiyo leo  Oktoba 19, 2025,  jijini Arusha.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bw Adolf Ndunguru,akipata maelezo i wakati akikagua  bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) katika Makao Makuu ya taasisi hiyo leo  Oktoba 19, 2025,  jijini Arusha.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »