WAKILI JUDITH KAPINGA APIGA HODI ARDHI YA TARAFA YA HAGATI

October 18, 2025


📍 *Mbinga-Ruvuma* 🇹🇿🌍


📌 *Ndugu.Kapinga aendelea kuomba Kura za CCM Kipapa*


📌 *Ndugu.Kapinga aeleza umadhubuti na Uimara wa CCM katika Utekelezaji wa Maendeleo*


📌 *CCM yaendelea kusaka Kura,yasisitiza Wananchi Oktoba 29 kupiga Kura*

Mgombea Ubunge Jimbo la Mbinga Vijijini kupitia tiketi ya CCM Wakili Judith Kapinga Octoba 17 Oktoba,2025 ameanza Ziara yake rasmi ya Kampeni ya kuomba Kura za CCM katika Kata ya Kipapa-Tarafa ya Hagati ametembelea Vijiji vya Matuta,Kipapa na Mhilo.

Katika Ziara hiyo, Kapinga ameendelea kuwashukuru Wananchi kwa mapokezi mazuri na moyo wao wa Upendo katika Mikutano hiyo,ameendelea kusisitiza sera yake kubwa ya kupita Kijiji kwa Kijiji ili ajionee Changamoto mbalimbali.Akiwa katika Vijiji hivyo.

Wakili Kapinga amepokea baadhi ya Changamoto mbalimbali za Maendeleo ameahidi kuzishughulikia na kuzisimamia kupitia Ilani  ya CCM ya Uchaguzi ya mwaka 2025/2030.

Katika,hatua nyingine Kapinga amewaeleza Wananchi umadhubuti na uimara wa CCM katika kuwaletea Maendeleo,hivyo amewaomba Kura za Kishindo kwa mgombea Urais wa CCM Dkt Samia Suluhu Hassan pamoja na mgombea mwenza Balozi.Dkt.Emmanuel Nchimbi.

Ndugu.Judith Kapinga ambaye ni Mgombea Ubunge Jimbo la Mbinga Vijijini na Ndugu.Essau Z.Ndunguru -Mgombea Udiwani Kata ya Kipapa.

Kwa Upande wa CCM,chini ya Mwenyekiti wa Timu ya Kampeni Jimbo la Mbinga Vijijini ambaye ni Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Mbinga Johnbosco Mkandawile ameendelea kuomba Kura za CCM na kusisitiza Wananchi kupiga Kura Oktoba 29 mwaka huu




         *Imetolewa na Ofisi ya Mgombea Ubunge Jimbo la  Mbinga Vijijini,Leo tarehe 18.10.2025*

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »