Na Mariam Kaagenda_Kagera
Mhandisi wa TANROAD, Johnston Mtasingwa ameibuka mshindi katika Uchaguzi wa Kura za maoni Jimbo la Bukoba Mjini kwa kupata kura 1,408 na kuwabwaga wenzake wanne waliokuwa wakishiriki mchakato wa kumpata Mbunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Bukoba Mjini, Shabani Mdohe ametangaza matokeo ya kura za maoni ambapo amewataja wengine waliogombea kuwa ni Alex Denis ambaye amepata Kura 804 , Almasoud Kalumuna kura 640 Jamila Hassan kura 66 na Koku Rutha kura 44
Wapiga kura waliojiandikisha ni 3033 waliojitokeza kupiga kura ni 2978 ambapo Kura zilizoharibika ni kura 20 na kura halali ni 2958.
EmoticonEmoticon