Mgombea Ubunge Jimbo la Ngara kupitia Chama cha Mapinduzi Dotto Bahemu amewaomba wanachama wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) kuvunja makundi na kuungana kwa Pamoja ili kukiwezesha chama hicho kupata ushindi wa Kishindo kwa Rais, Mbunge na Madiwani
Bahemu amesema hayo leo August 26 baada ya kuchukua fomu ya Uteuzi wa kugombea Ubunge Jimbo la Ngara katika ofisi ya msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ngara .
''Uchaguzi wa kura za maoni umeisha na kila mmoja alikuwa na kundi lake hivyo sasa ni jukumu letu sote kuungana kwa pamoja kutafuta kura za kishindo kwa Rais wetu, Mbunge na madiwani wote wanaotokana na chama cha mapinduzi"Alisema Dotto Bahemu.
Ameongeza kuwa atashirikiana na kila mtu hata ambao walikuwa hawamuungi mkono wakati wa uchaguzi wa kura za maoni na kati ya watu atakaoanza kuwatafuta na kuzungumza nao ni wale ambao walikuwa hawamuungi mkono na hawakuwa upande wake ili kujua tatizo liko wap huku akiwaomba wananchi wa Jimbo la Ngara kudumisha amani katika kipindi chote cha Uchaguzi.
Kwa upande wake Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Ngara Constantino Msemwa amesema kuwa Dotto Bahemu amekabidhiwa fomu hiyo baada ya kutimiza Vigezo na masharti yote.
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Bwana Ndaisaba Ruholo amesema atampatia ushirikiano wa Kutosha Dotto Bahemu katika kipindi chote cha Uchaguzi na kuwaomba wananchi na wanachama wa chama cha mapinduzi Jimbo la Ngara kumpa ushirikiano Mgombea aliyeteuliwa na Chama .
EmoticonEmoticon