DKT.DOTO BITEKO ACHUKUA FOMU KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA BUKOMBE

August 26, 2025


📌 Wanachama zaidi ya 1000 wajitokeza kumdhamini


📌 Dkt. Biteko ahimiza Kampeni za kistaarabu, mshikamano na upendo


📌 Awaomba Wana Bukombe kumchagua Dkt. Samia, Biteko na madiwani wa CCM


Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati


Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bukombe, Zedekiah Solomon Osan amemkabidhi fomu ya uteuzi wa kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Bukombe kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Doto Mashaka Biteko leo Agosti 26, 2025 katika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bukombe - Mkoani Geita.

Makabidhiano hayo ya fomu ni utekelezaji wa ratiba kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29 mwaka 2025 Aidha, Maelefu ya wana CCM na wapenzi wa chama hicho wamemsindikiza mgombea kwa ajili ya kuchukua fomu kwa ajili ya kuomba kuteuliwa na Tume huru ya Uchaguzi.

Katika hali isiyo ya kawaida, zaidi ya wanama 1000 wamejotokeza kumdhamini Dkt. Biteko ikilinganishwa na mahitaji ya wadhamini 31 waliohitajika kisheria.


Akiwa katika Ofisi za Tume, amekabidhiwa fomu hizo na  Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Bukombe Zedekiah Solomon Osano - 

Akizungumza na wanaCCM katika viwanja Ofisi ya CCM Wilaya ya Bukombe, Dkt. Biteko amewataka wananchi kudumisha mshikamano na upendo miongoni mwao na kuwachagua viobgozi bora.



“ Utakapofika wakati tuwaxhague viongozi tunaowapenda, nawaomba mmchague Dkt.  Samia Suluhu Hassan kuwa Rais, Mnichague mimi kuwa mbunge na niwaaombe mbiletee madiwani wa CCM kwa tuendeleze kazi tuliyokwisha ianza,” 

Awali, Katibu wa CCM, Wilaya Bukombe Leonard Mwakalukwa amesema wana CCM zaidi ya 3500 wamejitokeza kumsindikiza mgombea katika Ofisi za tume huru ya Uchaguzi kwa ajili ya kuchukua fomu.

Amesema  wadhamini 31 kutoka Kata zote 17 za Bukombe wamewawakilisha wenzao 969 waliojitokeza kumdhamini mgombea.




MWISHO

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »