KAMATI KUU CCM YAPEWA KONGOLE MCHAKATO UTEUZI WA WAGOMBEA

July 31, 2025

 


 Mfanyabiashara, Haidary Gulamali  akiwa katika moja ya mikutano yake ya chama.

................................

Na Dotto Mwaibale

KAMATI Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa chini ya Mwenyekiti wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imepongezwa kwa kumaliza mchakato wa uteuzi wa wagombea nafasi ya ubunge, udiwani na Ujumbe wa baraza la uwakilishi.

Jana Julai 28, 2025 kamati hiyo ilimaliza mchakato wa awali wa uteuzi wa nafasi ya kugombea Ubunge, Udiwani na baraza la uwakilishi katika Uchaguzi unaotarajiwa kufanyika oktoba mwaka huu.

Mchakato huo umepongezwa na wana CCM na wagombea wenyewe kufuatia hatua iliyochukuliwa na chama hicho ya kuifanyia marekebisho madogo katiba yake kwa kuomba ridhaa kwa wajumbe ya kuongeza idadi ya wagombea kutoka watatu hadi zaidi kulingana na kamati hiyo ilivyoona inafaa.

 Tayari mchakato wa uteuzi wa wagombea katika majimbo yote umekwisha kamilika na kutangazwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Mafunzo wa chama hicho Taifa, Amos Makalla.

Kinachofuata sasa ni kwa majina hayo kwenda kwa wajumbe kupigia kura na baadae kurudishwa mbele ya kamati hiyo kwa ajili ya kumpata mgombea mmoja katika jimbo husika.

Katika Jimbo la Ilongero mkoani  Singida wagombea saba wamechaguliwa ili wakapigiwe kura na wajumbe wa jimbo hilo.

Wagombe hao ni Ramadhani Abeid Ighondo mbunge aliyemaliza muda wake ambaye anatetea nafasi hiyo kwa kipindi cha pili, Lazaro Nyalandu ambaye alishawahi kuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia CCM ambapo, Aprili 30, 2021 alirejea tena CCM katika mkutano mkuu maalum wa chama hicho tawala  uliofanyika Jijini Dodoma.

 

Nyalandu alijitoa CCM Oktoba 30, 2017 akiwa Mbunge wa hilo zamani likiitwa Singida Kaskazini na baadaye kujiunga na Chadema ambako alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Kati. 

   Baada ya kuona kazi nzuri iliyofanywa na Serikali chini ya Rais Samia ndipo alipoamua kurejea CCM na mwaka huu wa uchaguzi ameamua kugombea tena nafasi hiyo kwa mara tatu.

Mgombea mwingine ni Mfanyabiashara, Haidary Gulamali ambaye amewahi kugombea nafasi hiyo kwa vipindi viwili lakini  ameingia kipindi cha tatu kujaribu bahati yake kwa mara nyingine kutokana na kuwiwa zaidi kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo.

Wengine waliochaguliwa na kamati hiyo kwa ajili ya kupigiwa kura na wajumbe ni pamoja na Mungwe Mgoo, Abdallah Haji, Maulid Sombi na Yustina Inyasi.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipokuwa akimkabidhi   nakala ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 mgombea ubunge wa CCM wa jimbo la Singida Kaskazini (ILONGERO), Ramadhan Ighondo, katika mkutano wa kampeni, uliyofanyika kwenye viwanja vya Ilongero, Septemba 15, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Lazaro Nyalandu akihutubia katika moja ya mikutano yake
 

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »