TANESCO YAANZA KUTEKEKEZA KWA KASI MPANGO KABAMBE WA UMEME BORA KIGAMBONI

March 22, 2025


Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeanza utekelezaji wa mpango kabambe wa kuimarisha njia za kusambazia umeme na kuongeza ubora wa Nishati ya Umeme katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa kiTANESCO wa Kigamboni. 


Mpango huu uliopewa jina la Umeme Bora Kigamboni umekuja baada ya maeneo ya baadhi ya maeneo ya Kigamboni kukumbwa na adha ya kukatika katika kwa umeme kulikosababishwa na ongezeko kubwa la mahitaji ya umeme pamoja na uchakavu wa miundombinu unaoathiri ufanisi wa utoaji wa huduma katika maeneo hayo.

Mpango huu  unalenga kutekeleza Miradi 35 ya kuboresha ubora wa nguvu za umeme yaani (Voltage Improvement Project) na unatarajiwa kukamilishwa sambamba na matengenezo makubwa kwenye njia 8 (Feeders) za kusambazia umeme.

Akizungumza katika moja ya maeneo ambayo TANESCO wanatekeleza Mradi Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Kifurukwe Ndugu Sultan Mbebe ameishukuru Serikali kupitia TANESCO kwa kuanza utekelezaji wa miradi hiyo kwani utasaidia kuondoa adha wanayoipata wakazi wa Kigamboni kwa sasa ya kukosa umeme wa uhakika.

Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni Bi Upendo Mahalu amelipongeza Shirika kwa hatua hiyo muhimu katika kuwezesha shughuli za kiuchumi katika wilaya ya Kigamboni. 



''Naipongeza Wizara ya Nishati kupitia TANESCO kwa kuja na mpango huu wa maboresho ya miundombinu ya umeme natoa rai kwa wananchi kuwa na uvumilivu watakapokosa huduma katika kipindi hiki cha mpito wakati TANESCO wakiendelea na maboresho hayo''


Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa wateja wa TANESCO Bi Irene Gowelle  amesema mpango huu ni wa muhimu ili kuimarisha hali ya umeme kwa wateja wao.


''Wakati wa utekelezaji Miradi hii wateja watakua wakikosa huduma katika vipindi vichache kwenye maeneo na siku tofauti ili kuwezesha kazi hiyo kufanyika hivyo Shirika linawaomba uvumilivu wateja wake ili kukamilisha kazi hiyo inayoendelea kufanyika.


Utekelezaji wa Mpango huu maalumu wa kuboresha hali ya upatikanaji umeme kwenye Mkoa wa KiTANESCO wa Kigamboni Unasimamiwa na Naibu Mkurugenzi Usambazaji wa umeme Mha. Athanasius Nangali akishirikiana kwa karibu na Wakurugenzi wa Kanda za Mashariki Mha. Kenneth Boymanda  na Kanda ya Nyanda za Juu kusini Mha. Sotco Nombo pamoja na Meneja wa Mkoa wa kiTANESCO wa Kigamboni Mha Paschal Luhwavi.


Wilaya ya  Kigamboni ni kati ya maeneo yanayokua kwa kasi ndani ya jiji la Dar es salaam hali inayosababisha uhitaji wa umeme kuwa mkubwa na wa muhimu kwa wananchi.

Share this

Related Posts

EmoticonEmoticon

:)
:(
=(
^_^
:D
=D
=)D
|o|
@@,
;)
:-bd
:-d
:p
:ng