Waziri wa Utalii na Mambo Kale wa Zanzibar, Mhe. Mudrick Soraga ametembelea Meza ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) wakati wa kongamano la Z-Summit lililofanyika Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA).
Kongamano la Z-Summit limefanyika kuanzia tarehe 19-20 Februari,2025 na kuwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya utalii ili kujadili changamoto na suluhisho za kuendeleza Zanzibar kama moja ya maeneo bora ya utalii duniani.
EmoticonEmoticon